Habari za Punde

Mbunge Sadifa aachiwa huru kesi ya rushwa

Mahakama ya Mkoa wa Dodoma imemwachia huru aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM na Mbunge wa Jimbo la Donge, Zanzibar, Sadifa Hamis,  baada ya Jamhuri kuwasilisha ombi mahakamani hapo la kuifuta kesi hiyo.

Katika shtaka la kwanza alidaiwa Desemba 9,2017 katika makazi yake kwenye Kata ya Mnada mjini Dodoma akiwa mwenyekiti wa Taifa wa UVCCM aliwahonga wanachama ili wamchague Rashid Mohamed aliyekuwa akiwania nafasi ya makamu mwenyekiti katika uchaguzi mkuu wa umoja huo.

Sadifa katika shtaka la pili alidaiwa katika eneo hilo na siku hiyohiyo, aliwaahidi kuwalipia usafiri wanachama wa umoja huo kuwasafirisha kutoka Dodoma hadi Kagera kama zawadi ili wamchague Rashid Mohamed aliyekuwa akiwania nafasi ya makamu mwenyekiti.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.