Habari za Punde

Hongera Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
Naibu Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe Hassan Khamis Hafidh ( Kulia) akiwa na Naibu Mkurugenzi Idara Habari MAELEZO Zanzibar, Dk Juma Mohammed Salum (Kushoto) wakimpongeza Abdallah Hassan Mitawi ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar. Kabla ya Uteuzi huo, Abdallah Mitawi alikuwa Katibu binafsi wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.
Mkurugenzi Idara Uratibu shughuli za SMZ katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Khalid Bakar Hamrani akimpongeza Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Abdallah Hassan Mitawi mara ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Abeid Amani Karume akitokea CUBA katika ziara Maalum na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe Balozi Seif Ali Iddi ( Hayupo pichani). Abdallah Mitawi ameteuliwa hivi karibuni kuwa Naibu Katibu Mkuu ambapo kabla ya Uteuzi huo alikuwa Katibu binafsi wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.