Habari za Punde

Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani na Uzinduzi wa Usafi na Utunzaji wa Mazingira Kwa Skuli za Unguja na Pemba Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.


Waziri wa Nchi Ofisi yaMakamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akizindua Kampeni ya Usafi na Utunzaji wa Mazingira Kwa Skuli za Unguja na Pemba, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani zilizofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akizindua kanuni ya sheria ya kudhibiti uingizaji wa mifuko ya Plastiki Zanzibar wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani zilizofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mihayo Juma  Nhunga na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ndg. Abdallah Hassan Mitawi wakishuhudia uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
Waziri Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akionesha Kanuni za Sheria za Udhibiti wa Mazingira baada ya kuizindua katika ukumbi wa mikutano wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar, ikiwa ni Siku ya Mazingira Duniani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akihutubia wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi na Wadau wa Mazingira Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akihutubia wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo June 5.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mihayo Juma Nhunga, akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mazingira Zanzibar Ndg Sheha Mjaja Juma akizungumza athari za mazingira zinazosababishwa na mifuko ya plasti katika jamii na adhabu yake ikiwa utapatikana na kosa hilo la kuingiza au kuuza mifuko hiyo na uharibifu wa mazingira katika maeneo ya makaazi ya Jamii na kadhalika.
Wageni waalikwa wakifuatilia hafla hiyo ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani zilizofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
Mkurugenzi Idara ya Elimu Michezo na Sanaa Ndg. Hairala Hassan Hairala akizungumza wakati wa maadhimisho hayo yaliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.