Mwakilishi Mkaazi wa UNFPA Tanzania Ms. Jacqueline Mahon, akitowa salimu za UNFPA katika Hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Idadi ya Watu Duniani Zilizoadhimisha Kitaifa Zanzibar katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
|
Assalaam Alaykum;
Habari za Leo!
Karibuni sana kwenye Siku ya Idadi ya
Watu Duniani
Ndugu Mgeni Rasmi, Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Ninayofuraha kubwa kuwakaribisha nyinyi nyote katika maadhimisho haya ya siku ya Idadi ya
Watu Duniani 2018 yakiwa na kauli mbiu
ya “Uzazi wa Mpango ni Haki ya
Binaadamu”. Huu ni ujumbe mzuri kabisa ambao unaendana na hali halisi ya masuala
ya Idadi ya watu katika nchi mbalimbali
duniani ikiwemo Tanzania.
Muhimu Zaidi ni
kwamba Siku ya Idadi ya Watu Duniani inalenga kupinga dhana ya kwamba uzazi wa
mpango ni kudhibiti Idadi ya Watu, baali ni kuhakikisha kuwa vizazi vyetu hawaichukulii
haki hii kwa mzaha. Pia siku hii inalenga kuimarisha haki za kidunia na mfumo
wa maendeleo ambao unaendana nao.
Ndugu Mgeni Rasmi, Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Miaka 50 iliyopita Mkutano wa Umoja wa Mataifa
kuhusu haki za Binaadamu, ulipitisha tamko mjini Teheran la May 13 1968
lililosema…na hapa ninanukuu “Wazazi wana haki ya msingi ya kuamua bila
kushurutishwa na kwa umakini idadi na mpishano wa watoto wao”- mwisho wa kunukuu. Wakitambulisha makubaliano yaliyofikiwa ujumbe
ulioratibu mapatano ulitangaza kwamba wamekubaliana Familia kujipangia wenyewe
na sio kupangiwa.
Uzazi wa mpango ni haki ya Msingi kwa wenza kuutumia, na sio kwa ajili ya kudhibiti Idadi ya Watu. Siku ya Idadi ya Watu Duniani mwaka huu 2018 imebeba ujumbe wa kuadhimisha
makubaliano haya ya Kihistoria.
Ndugu Mgeni Rasmi, Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Faida
zinazopatikana kupitia uzazi wa mpango ziko nyingi. Mojawapo nikuwa uzazi wa
mpango huwezesha upatikanaji wa njia za uzazi wa mpango kwa wenza na kwa
wanawake; hivyo ni muhimu sana kwa
ustawi wa mwanamke pamoja na kuimarisha Afya na maendeleo yake na jamii inayomzunguka..
Faida nyengine ni kama ifuatavyo:-
·
Uzazi wa mpango ni njia bora zaidi
kuliko njia nyengine zote za kufikia maendeleo ya dunia katika kupangilia hali
ya familia kwa masuala ya uzazi. Endapo
Wanawake na vijana watakuwa na fursa ya kupanga idadi ya watoto, lini, na kwa
mpangilio gani, basi wasichana wengi zaidi watabakia skuli kuendelea na
masomo na wanawake wengi wanaweza kuamua
kuingia ama kubakia katika sekta ya uzalishaji: Na bila shaka hapo tutaiona
familia nzima, jamii na nchi kwa jumla ikifaidika.
·
Kwa kila Dola moja inayotumiwa
kwa ajili ya Uzazi wa Mpango Serikali inaweza kuokoa mpaka jumla ya Dola sita
na hivyo kufanya uzazi wa mpango wa hiari moja ya uwekezaji bora Zaidi kufanya.
·
Pia kwa upande wa faida za kiuchumi na kijamii,
upatikanaji wa uhakika wa huduma bora za Afya ya uzazi zinakisiwa kuzalisha
faida ya Dola 120 kwa kila dola iliyowekezwa.
Ndugu
Mgeni Rasmi, Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana,
·
Uzazi wa
Mpango vile vile unaweza kusaidia nchi kufikia ‘demographic dividend’, - yaani ukuaji wa uchumi unaotokana na ongezeko la uzalishaji
linalotokana na ongezeko la watu wanaoingia kwenye shughuli za kiuchumi na
kupunguza utegemezi.
·
Vilevile Matumizi ya njia za uzazi wa mpango yanazuia zaidi ya theluthi
moja ya vifo vyote vya uzazi duniani kwa
kuwaruhusu wanawake kuchelewesha au kupangilia uzazzi, kuepuka mimba zisizohitajika na kuepusha utoaji mimba
usio salama.
·
Ufikiaji kamilifu wa mahitaji ya huduma za kisasa za uzazi wa mpango utapelekea kupungufu ya vifo sabini na sita elfu (76,000) vya uzazi kila mwaka pamoja nakupungua
vifo vipya vya uzazi laki nne na themanini (480,000)
·
Kuweza kupanga na kuchelewesha uzazi ni muhimu sana kwa
vijana baleghe chini ya miaka 18 ambao wako katika hatari kubwa ya vifo na
maumivu yatokanavyo na mimba za utotoni.
·
Kwa uande wa magonjwa ya kujamihiana: Kiwango kikubwa cha maambukizi ya
magonjwa ya kujamihina kipo kwa vijana
wa umri kati ya miaka 15 na 24. Hivyo Matumizi
ya njia za uzazi wa mpango hasa Condom za kiume na za kike yanatoa kinga mbili
kwa pamoja …yaani kinga dhidi ya mimba zisizohitajika na kinga dhidi ya
magonjwa ya kujamiina.
Mkazo wetu ni katika upatikanaji wa taarifa
na huduma kwa vijana baleghe na makundi mengine yaliyohatarini Zaidi.
Ndugu Mgeni Rasmi, Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Kufikia
maendeleo endelevu ya Dunia ifikapo mwaka 2030, itategemea sana ni kwa kiasi
gani haki ya Afya ya uzazi kwa wanawake na Vijana itatimizwa. Kutimiza mahitaji
yao ya Uzazi wa Mpango ni uwekezaji wenye faida kiujumla kuliko mwengine
Naomba
nimalizie kwa kusema kuwa UNFPA itaendelea kushirikiana na Serikali na wadau
wengine wa maendeleo kuhakikisha ‘’kuwa na Dunia ambayo kila ujauzito
unathaminiwa, kila uzazi ni salama na kila malengo ya kijana yanafikiwa’’.
No comments:
Post a Comment