Habari za Punde

Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Dkt. Khalid Mohammed Salum Akitembelea Eneo Linalotaka Kujengwa Mradi wa Ujenzi wa Maduka ya Kisasa Michezani wa ZSSF.

Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Dkt. Khalid Mohammed Salum, akizungumza na Maofisa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF, lipotembelea eneo linalotarajiwa kujengwa Maduka ya Kisasa katika eneo hilo la michezani Zanzibar. Ujenzi huo unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni baada ya kukamilika kwa mchakato wa kumpata mjenzi, kulia Kaimu Menaja Miradi na Uwezeshaji ZSSF Ndg. Abdulazizi Abrahaman Iddi, akitowa maelezo ya kitaalamu ya ujenzi wa majengo ya maduka katika eneo hilo, wakati wa ziara ya Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar.  
Kaimu Menaja Miradi na Uwezeshaji ZSSF Ndg. Abdulazizi Abrahaman Iddi, akitowa maelezo ya kitaalamu ya ujenzi wa majengo ya maduka ya kisasa katika eneo hilo, wakati wa ziara ya Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar. Mhe. Dkt. Khalid Mohammed Salum   


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.