Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Aifariji Familia ya Rajab Mgeni Kwa Kupata Ajali ya Kuunguliwa na Moto Nyumba Yao leo Asubuhi Rahaleo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud alipowasili katika eneo la  nyumba ilioungua kwa moto ya Familia ya Rajab Mgeni katika eneo la Rahaleo Unguja kutowa pole na kuifariji familia hiyo baada ya kupata mkasa huo.
Kwa mujibu wa wahusi moto huo umesababisha na hitilafu ya umeme kupitia chombo cha kuchemshia maji yamoto na kuleta shoti na kuteketele nyumba hiyo yote katika eneo la mbele lilikuwa na limehifadhiwa magodoro ya viti.
Katika ajali hiyo hakuna Mtu aliyejeruhiwa na kufariki moto huo umesababisha asara kubwa kwa mfanyabiashara ya viti vya makocho mali yake alikuwa amehifadhi katika nyumba hiyo na kuteketea kwa moto huo.  
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Naibu Waziri Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar. Mhe Shadya Mohammed alipowasili katika mtaa wa rahaleo kutowa pole kwa familia iliounguliwa na Moto Nyumba yao na kuteketeza mali iliomo ndani ya nyumba hiyo.kushoto Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Ndg. Makame Khatib Makame.  
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Wananchi wa mtaa wa rahaleo alipofika kuangalia ajali ya moto na kuwafariji familia ya nyumba hiyo iliopata majanga hayo leo asubuhi moto huo ulipotekea katika majira ya saa 2 asubuhi.kushoto Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Ndg. Makame Khatib Makame.  
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akipata maelezo kwa Maofisa wa Kikosi cha Uokozi na Zimamoto Zanzibar alipowasili katika eneo hilo la tukio la moto katika mtaa wa Rahaleo Unguja,Moto huo huo umetokea leo asubuhi na kusababisha hasara ya mali zilioko katika nyumba hiyo. 
Baadhi ya chumba katika nyumba hiyo vitu vyake vikiwa vimeteketea vyote kutokana na janga hilo la Moto uliotokea leo asubuhi katika moja ya nyumba ya Familia ya Mzee Rajab Mgeni rahaleo Zanzibar. 
Mabaki ya mabati ya nyumba hiyo ilioteketea yote kwa moto leo asubuhi na kusababisha asara kubwa kwa wakaazi wa nyumba hiyo.
Askari wa Kikosi cha Uokozi na Uzimaji wa Moto akiendelea na kuzima moto huo sehemu ya mabaki ya vifaa vilivyoungua moto katika janga hilo la moto lililotokea leo asubu katika mtaa wa rahaleo Zanzibar.
Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar wakiwa katika eneo la tukio wakihakikisha moto huo umezimika na kuzuia kuleta madhara kwa eneo hilo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akimsikiliza Kiongozi wa Familia ya Mzee Rajab Mgeni ni Kaka Mkubwa Mgeni Rajab akitowa ushuhuda wa janga hilo la moto lililoleta madhara makubwa katika familia yao na kusababisa hasara kubwa kwa kuungua kwa mali na vifaa vya wakaazi wa nyumba hiyo katikati mdogo wake Amour Rajab na kulia Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud. 
Sheha wa Shehia ya Muembeshauri akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi wakati wa tukio hilo la ajali ya moto lilillotokea katika shehia yake.katikati ni mmoja wa familia iliopata janga hilo Ndg. Amour Rajab. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na familia na Waandishi wa habari na kutowa pole kwa janga hilo la ajali ya moto wakati alipofika katika eneo la tukio hilo katika mtaa wa rahaleo Zanzibar leo asubuhi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud alipofika katika eneo la tukio la ajali ya moto katika mtaa wa rahaleo Unguja kushoto Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Ndg. Muhidini Ali Muhidini na kulia Mwakilisho wa Jimbo la Rahaleo Zanzibar Mhe. Nassor Salim Jazira. 
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya Maafa Zanzibar Ndg. Makame Khatib Makame na katikati Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Zanzibar Mhe. Nassor Salim Jazira, wakiwa katika eneo la tukio hilo la moto katika mtaa wa rahaleo Zanzibar.
Wananchi wakifuatilia tukio hilo la janga la moto katika mtaa wa rahaleo Zanzibar baada ya kumalizika kwa zoezi hilo la uzimaji wa moto huo, uliofanywa na Nguvu za Wananchi na Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar.
Wananchi wakifuatilia tukio hilo la janga la moto katika mtaa wa rahaleo Zanzibar baada ya kumalizika kwa zoezi hilo la uzimaji wa moto huo, uliofanywa na Nguvu za Wananchi na Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar. usilete majanga kwa maeneo jirani na tukio hilo.   

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.