Habari za Punde

Vyama Vya Siasa Vinavyoshiriki Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Jangombe Wasaini Maadili ya Vyama Vya Siasa.

Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Maadili ya Vyama vya Siasa katika Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Jang'ombe ambaye pia ni Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Mhe. Jaji Khamis Ramadhan Abdullah akisaini maadili ya vyama vya siasa wakati wa kikao Cha wajumbe wa kamati hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.    Wajumbe hao walikutana katika kikao hicho kwa ajili ya kusain maadili hayo ambayo yanalengo la kuweka utaratibu mzuri wa kuendesha Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Jang'ombe zikiwemo kampein za wagombea.  Jaji Ramadhan aliwataka wagombea kushirikiana pamoja katika kutekeleza maadili hayo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.