Habari za Punde

NAIBU WAZIRI KANYASU AIAGIZA HALMASHAURI YA BUCHOSA ITATUE MGOGORO WA ARDHI KATI YAO NA WANANCHI

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na wananchi  katika ziara ya siku mbili ya kutatua kero za wananchi mara baada ya kusikiliza malalamiko kutoka kwa  wananchi wa kijiji cha Bugombe kilichopo wilaya ya Sengerama mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanya  katika kijiji cha Bugombe wakiomba  waruhusiwe kutengeneza barabara ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Maisome ili kupunguza adha ya usafiri kwa wananchi hao.
Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Dkt. Charles Tizeba akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika ziara ya siku mbili ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu aliyoifanya ya   kutatua kero za  wananchi wa kijiji Bugombe  wilaya ya Sengerama mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanya  katika kijiji cha Kisaba na Bugombe
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu wakati alipofanya ziara ya kutatua kero za  wananchi wa kijiji cha Kisaba na Busikimbi vilivyopo wilaya ya Sengerama mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanya  katika kijiji cha Bugombe
Mwenyekiti wa Kijiji cha Bugombe akizungumza na na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika ziara ya siku mbili ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu aliyoifanya ya   kutatua kero za wananchi  wananchi wa kijiji cha Bugombe vilivyopo wilaya ya Sengerama mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanya  katika kijiji cha Kisaba na Bugombe
Daniel Serengeti ni mkazi wa kijiji cha Kisaba ambaye shamba lake limemegwa amemuomba Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu  amsaidie ili shamba lake lweze kurudishiwa kwa vile yeye ni mmiliki halali
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa amepanda kwenye bodaboda ukiwa ndo usafiri pekee unaotumika katika kijiji cha Bugombe ambayo ni kambai ya uvuvi kutokana na kukosekana kwa barabara ya kuweza kupita magari.                               
                               (Picha na Lusungu. Helela)                                                            

Na.Lusungu Helela -Mwanza.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ameiagiza Halmashauri ya wilaya Buchosa mkoani Mwanza kupitia upya ramani ya vijiji vilivyopo ndani ya   Hifadhi ya Msitu wa   Kisiwa cha Maisome kwa ajili ya kutatua mgogoro wa ardhi  uliopo kati ya wanavijiji na Halmashauri hiyo.
Ameuagiza Uongozi wa Halmashauri hiyo ushirikiane na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)  wakati wa inapofanya upya mapitio ya ramani hiyo ili kuweza kumaliza tatizo la mgogoro huo uliopo kufuatia baadhi ya maeneo ya wananchi kuingia ndani ya  Hifadhi ya msitu huo kwa mujibu ramani iliyopo.
Ametoa agizo alipokuwa wilayani humo kwa ziara ya siku mbili ya kutatua kero za wananchi mara baada ya kusikiliza malalamiko kutoka kwa  wananchi wa kijiji cha Kisaba na Busikimbi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanya  katika kijiji cha Kisaba wakidai kuwa TFS imechukua baadhi ya maeneo ya vijiji hivyo.
Katika vijiji hivyo  jumla ya ekari 103 za   wananchi walizokuwa wakizitumi katika shughuli za kiuchumi zinadaiwa kuingia ndani ya Hifadhi ya msitu iliyo chini ya TFS
Naibu Waziri Kanyasu amefafanua kuwa hakuna mgogoro kati ya TFS na wananchi ila kuna mgogoro kati ya wananchi na Halmashauri waliotengeneza ramani hiyo na sio TFS.
Daniel Serengeti ni mkazi wa kijiji cha kisaba ambaye shamba lake limemegwa ameiomba serikali kuwarudishia maeneo hayo kwa kuwa walikuwa wanayamiliki tangu mwaka 1968.
‘’ wachora ramani sio TFS, Hivyo TFS wanatumia ramani iliyokwisha tengenezwa  na Halmashauri hiyo kutokana na hilo wanatakiwa kupitia upya na kuondoa mgogoro,alisema .Kanyasu.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Buchosa Crispin Luanda amesema kuwa maagizo hayo atayatekeleza kwa wakati ili kufanikisha swala hilo .
Amesema mara baada ya ramani mpya itakapokamilika  itapelekwa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ajili ya urekebishaji wa maeneo hayo.
Katika hatua nyingine,  Kanyasu ameruhusu upanuzi wa njia itakayopita ndani ya Hifadhi ya Maisome kwa ajili ya kuwapunguzia adha  wakazi  walio wengi wanaokwenda katika Kambi ya Uvuvi ya Bugombe kwa ajili ya kujipatia mahitaji muhimu ya kila siku.
Mbunge wa jimbo la Buchosa Dk Charles Tizeba amemshuru naibu wa Waziri huyo kwa kutatua mgogoro huo ambao ulikuwa kero kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.