Habari za Punde

Elimu Inayotolewa Visiwani Inaandaa Vijana Kuuzika Nje ya Tanzania.

Na Masanja Mabula –Pemba……..24/01/2019.
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imesema mfumo wa elimu inaotolewa visiwani ni bora kwani inawaandaa vijana kuuzika  ndani ya nje ya Tanzania.
Ofisa Mdhamini wizara ya Elimu Pemba Ndg.Mohammed Nassor Salim akizungumza kwenye kikao cha maafisa elimu wilaya pamoja na wakurugenzi wa Halmashauri na Mabaraza ya Miji Pemba , amesema ushahidi wa hayo ni wanafunzi wa Zanzibar kufanya vyema katika vyuo mbali mbali.
Amesema ni vyema maafsa elimu na wakurugenzi kusimamia ili kuona mfumo huo bado unaendelea kuleta tija kwa vijana.
“Mfumo wetu wa utoaji wa elimu bado uko bora, kwani vijana wanaotoka  Unguja na Pemba wanafanya vyema katika vyuo mbali mbali vya ndani ya nje ya nchi”alifahamisha.
Ofisa mdhamini ametumia fursa hiyo kuwataka maafisa elimu na wakurugenzi kuendelea kuwasimamia walimu na kuwafanya wawe wazalendo wa nchi yao.
Makamo mwenyekiti wa baraza la Mji Mkoani Mshenga Haji Khamis  akizungumza kwenye kikao hicho, amewashauri walimu kufanya kazi kwa kujituma ili kuwafanya wanafunzi kuingia katika ushindani wa soko la ajira wakiwa wameandaliwa vyema.
Amesema  pamoja na serikali kuweka mazingira na miundo mbinu , lakini wapo baadhi ya walimu wanajihusisha na siasa sehemu za kazi zao, jambo ambalo linapelekea matokeo mabaya ya wanafunzi.
“Nambatua wapo baadhi ya walimu wanasahau majukumu yao na badala yake wanashughulikia siasa na hivyo kupoteza vipindi vingi na wanafunzi kukosa masomo”alieleza.
Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Micheweni Omar Issa Kombo ameeleza kuridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuimarisha miundo mbinu ya kujifunzia.
Amesema madarasa mengi yamejengwa na mengine yanaendelea kujengwa kupitia nguvu za wananchi pamoja na serikali, jambo ambalo limeweza kusaidia kuondoa tatizo la upungufu wa vyumba vya kusomea.
“Hakika serikali imefanya mengo za ziada katika kuimarisha sekta ya elimu, hii imesaidia kuwafanya wanafunzi kuwafanya kuwa rafiki wa mazingira ya kujifunzia”alifahamisha.
Hivyo amewataka wananchi bila kujali itikadi zao , washirikiane na serikali kupitia wizara ya elimu na Mafunzo ya Amali katika kusimamia suala la uboreshaji wa elimu nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.