Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Jijini
Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza na watumishi wa
mamlaka hiyo mara baada ya kufanikiwa kupata tuzo hiyo kulia ni
Afisa Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira
Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Haika Ndalama akizungumza wakati wa halfa
hiyo
Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Dorrah Killo akizungumza wakati wa halfa hiyo |
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi
wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akiwa
amebebwa na watumishi wa mamlaka hiyo wakimpongeza baada ya kupata
tuzo hiyo
Watumishi wa mamlaka hiyo wakiwa na tuzo hiyo
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Jijini
Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kushoto ambaye amevaa koti
akiwa na watumishi wa mamlaka hiyo wakisheherekea ushindi wa tuzo hiyo
Watumishi wa Mamlaka hiyo wakicheza kwa furaha baada ya kupata
tuzo hiyo
Watumishi wa mamlaka hiyo wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye
halfa hiyo
Watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini
Tanga (Tanga Uwasa) wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye halfa hiyo
Msafara wa magari na pikikpiki ukitokea eneo la Pongwe Jijini
Tanga wakielekea Ofisi za Mamlaka ya Maji Jijini Tanga mara baada ya
mapokezi ya tuzo hizo
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)
imepata tuzo kwa kuwa mamlaka bora katika utoaji wa huduma za maji
safi kwa mamlaka za mikoa 25 Tanzania kwa mwaka 2017/2018.
Tuzo hiyo ilitolewa na Mamlaka ya Udhibiti Nishati na Maji nchini
(EWURA) kutokana na utendaji kazi wao na utoaji wa huduma baada ya
kufanya tathimini na hivyo kujikuta wakifanikiwa kuigia kwenye nafasi
hiyo ya kuny’akua tuzo hiyo.
Akizungumzia namna walivyopokea tuzo hiyo baada ya mapokezi makubwa
yaliyoanzia eneo la Pongwe Jijini Tanga Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji
safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey
Hilly alisema wanafurahi kutokea tuzo hiyo kmuwa mamlaka bora katika
huduma ya maji safi kati ya mamlaka 25 Tanzania bara ni faraja kubwa
sana kwao.
Alisema wameipata tuzo hiyo kwa sababu wamekuwa na nia ya kuipata
kutokana na ufanisi mkubwa wa kufanya kazi kwa bidii kwa maarifa huku
wakijua vigezo vinavyotakiwa na vigezo kwa ujumla wake ni ubora wa
huduma kwa wananchi wanapata maji muda wa kutosha na maji bora.
Alisema pia ni kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama maji
kwa kuwafikia watu wengi iwezekanovyo huku wakipunguza upotevu wa maji
ambayo vimechangia wao kuonekana mamlaka bora ya kwanza Tanzania bara
kutoa huduma ya maji safi 2017/2018,
Mkurugenzi huyo alisema baada ya kupata tuzo hiyo hivi sasa mikakati
yao ni kuendelea kujipanga kutambua jinsi vigezo vinafanyiwa kazi ili
kupata mamlaka bora kila mwaka kutokana na utoaji wa huduma bora kwa
wananchi.
“Tumejipanga na Tutatekeleza yale yanafanyika kwenye vile vigezo
tuendelee kubaki kuwa mamlaka bora Tanzania bara na ulimwengu mzima
kama ilivyo malengo yetu “Alisema Mkurugenzi huyo.
Awali akizungumza katika halfa hiyo Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo
Dorrah Killo alisema baada ya kupata tuzo hiyo wataendelea kupambana
kuhakikisha wanaendelea kung’ara katika utoaji wa huduma hapa nchini
“Tukienda mwakani vigezo zinaweza kuwa vikubwa hivyo tutaendelea
kujipanga lakini niwaambie kwamba tumewatupa mbali sana wenzetu
waliokuwa karibu nasi..hii inatokana na jitihada kubwa za bodi ya
wakurugenzi,uongozi na wateja wao”Alisema Afisa Uhusiano huyo.
Alisema suala linguine ni kuwahudumia wateja wao vizuri kwani bila
kuwahudumia wateja na kutoa elimu nzuri kwao wasingeweza kufikia hatua
hiyo wanashaukru wateja wao na wafanya kazi kwa bidii washirikiana
wapendani ili kufikia malengo yao.
No comments:
Post a Comment