Habari za Punde

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Magufuli Arejea Nchini Akitokea Nchini Afrika Kusini, Namibia na Zimbabwe leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Brigedia Jenerali  Abdallah M. Alphonce na wafanyakazi wa ubalozi huo Bi. Alice Madele na Bi Joyce Makoye katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Mugabe jijini Harare,  kabla ya kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kurejea nyumbani akitokea Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya
siku mbili kwa kila nchi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe Mhe. Dkt. Emmerson Mnangagwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Mugabe jijini Harare leo alhamisi Mei 30, 2019 baada ya kuhitimisha ziara yake ya Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe
ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akitelemka kutoka katika ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Alhamisi Mei 30, 2019 akitokea Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya
ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna wa Polisi Diwani Athumani baada ya kutelemka kutoka katika ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo alhamisi Mei 30, 2019 akitokea Afrika Kusini
alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo alhamisi Mei 30, 2019 akitokea Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa
wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda
Picha na Ikulu.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.