Habari za Punde

Naibu Meya Mhe Joseph Lyata Atatua Tatizo la Barabara ya Dodoma Road.

NAIBU Meya Manispaa ya Iringa Joseph Lyata kwa kushirikiana na Chama cha Mapinduzi CCM Manispaa wameendelea kutekeleza ahadi ya kukarabati za Mitaa iliyopo kata ya Mtwivila kama ambavyo unawaona hapo kwenye picha
NAIBU Meya Manispaa ya Iringa Joseph Lyata akiwa anaangalia ukarabati barabara za Mitaa iliyopo kata ya Mtwivila
Baadhi ya watoto na wananchi wakiangalia ukarabati wa barabara ukiendelea katika mitaa ya kata ya Mtwivira

Na.Fredy Mgunda - Iringa.
NAIBU Meya Manispaa ya Iringa Joseph Lyata kwa kushirikiana na Chama cha Mapinduzi CCM Manispaa wameendelea kutekeleza ahadi ya kukarabati za Mitaa iliyopo kata ya Mtwivila.

Akizungumza na wananachi wa Mtaa wa Dodoma Road C wakati wa kukarabati barabara hizo, Lyata amesema kuwa wameamua kukarabati barabara hiyo kutokana na ubovu uliokuwepo awali.

Lyata amesema kuwa anashangaa kuona Diwani wa kata ya Mtwivila kushindwa kukarabati barabara za mitaa hiyo huku akiwataka wananchi wa Kata hiyo kutoa taarifa katika ofisi yake na kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili.

Awali Lyata amebainisha kuwa Chama cha mapinduzi kimekuwa kikiwafikia wananchi wa chini na kujua changamoto zao na kisha kuzitatua.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa DODOMA ROAD C Mzee Said Mwachang’a amemshukuru naibu meya manispaa ya iringa Joseph Lyata kwa kuwarekebishia barabara hiyo kwani itafungua fursa ya wafanyabiashara kufika katika mitaa yao.

“Nikushukuru Naibu meya kwa kuja kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kwani umeonesha wewe ni kiongozi wa watu na tunakupongeza kwa hili” alisema Mwachang’a

Nao baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Dodoma Road C wamebainisha kuwa baada ya ukarabati wa barabara hiyo utapelekea waweze kufanya shughuli zao bila tatizo.

Lakini diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Chengula alisema kuwa chama cha mapinduzi na naibu meya wa manispaa ya Iringa walikuwa hawalali kwa ajili ya kutatua tatizo la barabara ya Dodoma Road  kwa kuwa wananchi hao wanahitaji kufanya kazi za kimaendeleo

“Wananchi wa kata ya Dodoma Road wanahitaji kufanya maendeleo kwa kuwa wamekuwa wachapa kazi wakubwa lakini mbunge wao amekuwa hawasaidie kwa lolote hivyo ndio chama na Naibu Meya walipobebe jukumu la kutatua changamoto hiyo” alisema Chegula

Chegula alisema kuwa kipaumbele kilikuwa kutatua changamoto ya barabara ndipo wanatafuta njia nyingine ya kutatua changamoto nyingine zilizopo katika mtaa wa Dodoma Road ili wananchi wafanye kazi kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anavyotaka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.