Habari za Punde

Skuli ya Sekondari ya Tumekuja Yafanya Sherehe za Maghafali ya 12 ya Kidatu cha Sita Mjini Zanzibar.

Mgeni Rasmin Shamaame Shamata akimkabidhi Cheti Mwanafunzi bora aliyefaulu Masomo yote Skuli ya Tumekuja Yussuf Salum Khamis (Kulia) ni Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Tumekuja Khamis Mngwali Mshenga.
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ  Zanzibar Mh. Shaame Shamata Khamis amewtaka wanafunzi waliyohitimu  masomo yao kutojiingiza katika makundi maovu na kushughulikia kazi zitakazowaletea maendeleo katika maisha yao.
Ameyasema hayo katika Maaghafali ya 12 baada ya kuwakabidhi zawadi wahitimu wa  kidato Sita huko  Skuli ya Tumekuja iliyopo Mjini Zanzibar.
Ameseama  ni vyema wahitimu hao kuwamakini katika kujitafutia maendeleo jambo ambalo litawaletea msingi bora wa maisha yao.
Aidha  Mh. Shaame amesema Serikali imejitahidi kutoa Vifaa mbalimbali  katika Sekta ya Elimu ili kuwapatia taaluma ilyobora na kupata wataalamu wengi Nchini.
Hata hivyo amewomba Wazazi kuendelea kutoa mashirikiano kwa walimu ili kuondokana na changamoto zinazowakabili wanafunzibili wanafunzi wao hasa katika kipindi cha mitihani inapokaribia.
Nae Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Tumekuja Khamis Mngwali Mshenga amesema wameamua kuiga kuanzisha somo jipya mwaka huu lenye kambinesheni ya Chemisty Biology and Methimetic (CBM) jambo ambalo litawaletea faraja katika Wanafunzi hao katika masomo yao.
Pia amesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali  katika Skuli yao ilikiwemo Maji, Mashine ya Kupirintia karatasi za Mitihani na Uhaba wa Madarasa wakati wanayofundishia wanafuzi hao jambo ambalo linawakoseaha faragha katika kazi utowaji wa Elimu hio.
Kwa upande wao wahitimu hao wamesema wameahidi watayafanyia kazi yaleyote waliyoambiwa ilikuepukana na matatizo yanayoweza kuepukika katika jamii yao.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.