Mkaguzi wa chakula Mwandamizi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania TFDA Dkt Analice Kamala wakati akiwasilisha mada juu ya uchafuzi wa Sumukuvu madhara yake kwa afya na jinsi ya kudhibiti katika Semina ya kuwajengea uwezo Waandishi na Wahariri wa Habari katika kuelimisha jamii kuhusu usalama wa chakula iliyofanyika Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
Na.Grace Semfuko,MAELEZO
Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania TFDA imesema inayo maabara
ya kisasa ya upimaji wa usalama wa mazao ya Chakula ili kuondokana madhara
yatokanayo na ulaji wa vyakula vizivyopimwa yakiwepo magonjwa yanayotokana na
ulaji wa vyakula vyenye Sumu kuvu.
Aidha Mamlaka hiyo imejipanga kupambana na magonjwa
yanayosababishwa na ulaji wa vyakula hivyo ambayo yana athari kubwa kwa afya za
binaadamu ikiwepo udumavu na vifo.
Hayo yalibainishwa na Mkaguzi wa chakula Mwandamizi wa Mamlaka
ya Chakula na Dawa Tanzania TFDA Dkt Analice Kamala wakati akiwasilisha mada
juu ya uchafuzi wa Sumukuvu madhara yake kwa afya na jinsi ya kudhibiti katika
Semina ya kuwajengea uwezo Waandishi na Wahariri wa Habari katika kuelimisha
jamii kuhusu usalama wa chakula iliyofanyika Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
Dkt Kamala alisema alisema maabara za kisasa za upimaji wa
vyakula zilizopo kwenye Mamlaka hiyo zina uwezo wa kisasa wa kubaini magonjwa
au vimelea vya fangas ambavyo huathiri vyakula hususa vilivyohifadhiwa kwenye
maeneo yasiyo salama ikiwepo sehemu ya
unyevu unyevu,joto na wadudu wa nafaka.
“ Niwahakikishie tu watanzania wenzangu kuwa vyakula
vinavyopimwa kwenye maabara hii ni salama, hakuna kinachopita hapa kikiwa na
madhara, kitatupwa tu, tuzingatie usalama wa vyakula na tutumie vyakula
vilivyopimwa alisema Dkt Kamala.
Aidha katika hatua nyingine Dkt Kamala aliwataka Wanawake
wanaonyoshesha nchini kuwa waangalifu katika uandaaji na matumizi ya vyakula
wanavyotumia ili kuepukana na madhara ya Sumukuvu iliyopo kwenye baadhi ya
vyakula vya nafaka ambayo inadaiwa kuwa na madhara kwa binaadamu na wakati
mwingine husababisha vifo.
Dkt Kamala alisema iwapo Mama anayenyonyesha atatumia vyakula
vyenye sumukuvu anasababisha madhara makubwa kwa Mtoto ikiwepo Udumavu, Vifo na
Magonjwa ambayo yanaathiri ukuaji wa mtoto.
“Wanawake wanaonyonyesha ni muhimu kuzingatia uandaaji wa
vyakula kwani watoto hula vyakula hivyo kupitia kwenye Maziwa ya Mama na hivyo
kuathiri mfumo mzima wa ukuajiälisema Dkt Kamala.
Aidha pia Dkt Kamala alisema ulaji wa mazao ya mifugo
iliyotumia vyakula vilivyoathiriwa na sumu kuvu pia inaweza kuathiri afya za
binaadamu.
Alisema Sumu kuvu inaathiri ini na Figo na kusababisha ugonjwa
wa manjano na wakati mwingine kuvuja damu kwenye maeneo ya wazi,kuharisha na
kuhisi kichefuchefu na dalili zake huanza kuonekana baada ya wiki mbili.
Ugonjwa huo kwa
Nchini Tanzania ulilipotiwa na Wizara ya Afya Juni 13 mwaka 2016 Mkoani Dodoma
ambapo ilibainika kuwepo kwa watu 68 kwenye familia 42 kuugua magonjwa
yatokanayo na ulaji wa vyakula vyenye sumu kuvu na kati yao watu 20 sawa na
asilimia 30 walipoteza maisha.
No comments:
Post a Comment