Habari za Punde

Ubalozi Mdogo wa Chana Zanzibar Wakabidhi Msaada wa Vifaa na Vyakula Kwa Watoto wa Nyumba ya Watoto Mazizini Zanzibar.

Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Maudline Cyrus Castico (kushoto) akiwa na Mke wa Balozi Mdogo wa China Zanzibar Mama Liu Jie wakitembelea nyumba ya kulelea watoto yatima Mazizini alipofika kutoa misaada ya vitu mbalimbali.
Mke wa Balozi Mdogo wa China Zanzibar Mama Liu Jie akizungumza na watoto yatima wanaolelewa kwenye nyumba ya serekali iliopo Mazizini alipofika kutoa msaada wa vitu mbalimbali, ikiwa ni miongoni mwa shamrashara za kuelekea siku ya watoto wa Afrika zitakazoazimishwa juni 16.
Mke wa Balozi Mdogo wa China Zanzibar Mama Liu Jie akikabidhi kopo la Maziwa ikiwa ni moja ya msaada aliotoa kwa watoto yatima wanalelewa katika nyumba ya Serekali iliyopo Mazizini Mjini Zanzibar.
Mke wa Balozi Mdogo wa China Zanzibar Mama Liu Jie akikabidhi kopo la Maziwa ikiwa ni moja ya msaada aliotoa kwa watoto yatima wanalelewa katika nyumba ya Serekali iliyopo Mazizini Mjini Zanzibar.
Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Maudline Cyrus Castico na Mke wa Balozi Mdogo wa China Mama Liu Jie katika picha ya pamoja na watoto yatima.

Picha na Makame Mshenga.
Na. Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar.
Ubalozi mdogo wa China ulipo Zanzibar umekabidhi msaada wa Chakula na Vifaa mbalimbali kwa Watoto wanaoishi nyumba ya kulelea Watoto Mazizini ikiwa ni mwendelezo wa kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia wa muda mrefu katika ya Tanzania na Jamhuri ya watu wa China.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Mabegi ya Shule, Kalamu, Madafatari, Mipira ya kuchezea, Maziwa, Sabuni na Manukato ili visaidie kuwafariji Watoto hao kuelekea siku kuu ya Idd na maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika.
Akikabidhi Msaada huo kwa niaba ya Ubalozi wa China Mke wa Balozi wa China Mama Liu Jie amesema nchi rafiki wa China zimeongezeka duniani lakini kamwe China haiwezi kuisahau Tanzania ambayo imekuwa rafiki wa muda mrefu.
Amesema China itaendeleza uaminifu wake wa kisiasa na Tanzania na kushirikiana katika nyanja za kiuchumi na biashara.
Mama Lui ameongeza kuwa China itazidisha nguvu ya misaada kwa Tanzania kwa lengo la kuwasaidia wananchi wake kuishi kwa furaha na amani.
“Miaka ya 1970 ambapo uchumi wa China ulikuwa mdogo tuliweza kusaidia kujenga Reli ya TAZARA, hivyo tutaendelea kusaidia mambo mengine muhimu katika kipindi hiki ambapo uchumi wa China umekuwa na kuwa Taifa la Pili duniani kiuchumi.” Alisema Mama Lui.
Kwa upande wake Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Moudline Cyrus Castiko ameishukuru China kwa kuendelea kuisadia Tanzania katika Nyanja mbali mali za kimaendeleo.
Amesema Watoto ni nguvu kubwa ya kujenga Makabila na Taifa hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuwasaidia ili kutimiza malengo yao.
Amempongeza Mke wa Balozi huyo wa China kwa misaada mbali mbali anayoitoa kwa Watoto ambapo mwaka 2017 akiwa na Mke wa Rais Shein waliletea Vyakula, Vifaa vya kusomea na kupima afya za Watoto kituoni hapo.
Waziri Castiko ametoa wito kwa jamii kutoa misaada ya mahitaji kwa Watoto wanolelewa katika kituo hicho cha Mazizi ili kuwafariji.
“Kila mtu anahitaji kuguswa na watoto hawa ambao hawana Wazazi na wito wangu anayetaka kuwasaidia aje kituoni ili awasaidie, kwa wale wasio na uwezo hata kuwapa Mayatima hawa maneno ya faraja ni msaada mkubwa kwao” aliongeza Mama Castiko.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa amesema kituo hicho cha kulelea Watoto kwa sasa kina jumla ya Watoto 30 ambapo kati yao 16 ni Wasichana na 14 ni Wavulana.
Amesema Watoto hao wanahitaji kupendwa na kutiwa moyo ili watakapokuwa watu wazima nao waweze kuwa na upendo wa kuihudumia wenzao na nchi kwa ujumla.
Urafiki wa Jamhuri ya Watu wa China na Tanzania una historia ndefu inayoimarishwa kila leo ambapo huu ni mwaka wa 55 tangu nchi hizo zianzishe uhusiano wa kidiplomasia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.