Habari za Punde

Innaa lillaahi Wainnaa ilayhi Rajiuun. Buriani Msanii Mkongwe Bi Khadija Baramia


Msanii gwiji wa zamani wa nyimbo za taarab Zanzibar Marehemu Bi. Khadija Baramia . aliyefariki dunia akiwa Nchini Oman  alipokuwa akipata matibabu.

Marehemu Baramia alipata umaarufu Zanzibar katika sanaa ya taarab kwa kuimba katika vikundi mbalimbali kikiwemo cha Nuru Luyun kilichojizolea sifa nyingi katika miaka ya 1980 akiwa ni miongoni mwa waazilishi wa kikundi hicho.

Nyimbo ambazo zilizomzolea sifa wakati wa uhai wake ni pamoja na Mapenzi yako matamu,Madhulumu Moyo, Wacheni kulia Wivu,Pendo la Moyoni Bustani Njema, Nimezama kwenye huba lako,Wadhinifu Kisima na Dunia ina fisadi.

Marehemu Bi. Khadija Baramia anatarajiwa kuzikwa leo baada ya Sala ya Ijumaa  maziko yatafanyika Kikwajuni Weles Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.