Habari za Punde

RC Kusini Unguja afungua Baraza la Mkoa pamoja na kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM

 Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud akizungumza na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)kuhusu mashirikiano ya Jumuiya hiyo huko Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kusini Unguja.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi  (NEC) Semeni Khamis Vuai akizungumza kuhusu Mashirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud (hayupo Pichani) huko Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kusini Unguja.
 Baadhi ya Wanajumuiya ya  Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wakimsikiliza kwa makini  Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud  (hayupo Pichani) huko Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kusini Unguja.
 Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud akionyesha Zawadi ya Cheti alichopewa kutoka Wilaya ya kati baada ya kuskiliza  Taarifa ya utekelezaji wa Kazi ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kati Unguja kwa kipindi cha January hadi June 2019
 Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja Hamida Mussa Khamis akitoa Taarifa kuhusu utekelezaji wa Kazi ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kati Unguja kwa kipindi cha January hadi June 2019 
 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kati Unguja Salma Omar Said akisoma Muhtasar wa Utekelezaji wa Kazi ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kati Unguja kwa kipindi cha January hadi June 2019 huko Dunga Mkoa wa Kusini Unguja .
 Baadhi ya Watendaji kutoka Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja wakifatilia kwa makini Taarifa ya utekelezaji wa Kazi ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kati Unguja kwa kipindi cha January hadi June 2019.
 Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud akiskiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja Hamida Mussa Khamis kuhusu Ujenzi wa Nyumba ya Mama mwenye Watoto walemavu katika Nyumba hiyo Dunga Wilaya ya Kati Unguja.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud akizungumza na Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Kusini Unguja kuhusu kujua tasmini ya hali ya Uasalama katika Mkoa huo, huko Ofisini kwake Tunguu.

Picha na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.

Na Mwashungi Tahir    Maelezo     29-9-2019
Mkuu wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud ameahidi kufanya kazi kwa mashirikiano  kwa lengo la kuleta mageuzi na maendeleo makubwa katika Mkoa huo.
Akizungumza na viongozi mbali mbali wa Mkoa huo huko katika Ofisi ya Wilaya ya Kati Dunga wakati alipokuwa akipokea taarifa za utekelezajiwa kazi ya chama cha Mapinduzi  wilaya ya kati Unguja kwa kipindi cha January hadi Juni 2019.
Amesema iwapo watashirikiana na kufanya kazi kwa pamoja na viongozi wenziwe  basi atahakikisha Mkoa huu utakuwa na mafanikio ya hali ya juu na mambo mengi ya  maendeleo yataweza kuonekana na kuwataka wananchi watarajie fursa mbali mbali .
Ameahidi kukaa pamoja na wananchi kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuweza kutekeleza majukumu yake kwa kuzitatua shida hizo na kuzipatia ufumbuzi.
“Nitakuwa na mpango maalum wa kukaa na wananchi wa Mkoa huu ili wanieleze changamoto zao na kuweza  kuzifanyia kazi kwa kuzitatua”, alisema Mkuu wa Kusini Ayoub.
Aidha amesema atahakikisha amani iliyopo ndani ya Mkoa huo itaendelea kuwepo kwani bila ya kuwepo amani hatutoweza kufanya kazi kwa ufanisi.
Pia ameahidi kuhusu suala la elimu la watoto kufaulu mitihani yao atalishughulikia kwa nguvu zote na kuhakikisha wanafunzi wanapasi masomo yao kwa vizuri ndani ya Mkoa huo.
Ayoub ameridhishwa na suala la Malaria katika Wilaya ya kati kuwa imepungua sana baada ya nyumba nyingi kupigwa dawa wakati hapo zamani ilikuwa kubwa na kuwataka wananchi kutoa mashirikiano katika suala la kuimarisha afya zao.
Wakati huo huo Mkuu wa Kusini alizungumza na kamati ya ulinzi na usalama huko ofisini kwake Tunguu Mkoa wa Kusini na kuwataka kuongeza nguvu sehemu ambayo itakuwa haikuwa sawa ili wananchi waweze kuishi kwa amani.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Kati Hamida Mussa Khamis akitoa taarifa ya Utekelezaji wa kazi amesema hali ya usalama katika Wilaya ni ya kuridhisha .
Pia amesema changamoto uuzaji na upikaji wa pombe za kienyeji  katika wilaya hiyo , suala la udhalilishaji na ukosefu wa vyoo katika baadhi ya Skuli zote hizo watashirikiyana kuzitatua .
Sambamba na hayo Salma Omar Said Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya kati akitoa taarifa ya Utekelezaji amesema tayari wameweka mkakati wa kupata ushindi katika Chama cha Mapinduzi ifikapo 2020 na kuahidi itashinda kwa kishindo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.