Habari za Punde

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan Atembelea Eneo Walilozikwa Wahanga wa Ajali ya Kivuko Cha MV.Nyerere na Kufungua Kituo Cha Afya Ukara

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu Hassan, akiweka Shada la Maua kwenye Mnara wa kumbukumbu  Eneo walipoozikwa Wahanga wa Ajali ya Kivuko cha MV Nyerere Kisiwani  Ukara Wilayani Ukerewe leo Disemba 14,2019 wakati malipotembekea Eneo hilo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu Hassan, akikata utepe kuweka Jiwe la Uzinduzi wa Majengo mapya ya Kituo cha Afya  Bwisya Ukara Ukerewe 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu Hassan, akimpa pole Mtoto Femia Sabato (3)mkazi wa Bwisya Ukara aliyelazwa katika  Kituo cha Afya  Bwisya Ukara kwa matibabu mara baada  kuzinduzi wa Majengo mapya ya Kituo cha Afya  Bwisya Ukara Wilayani Ukerewe leo Disemba 14,2019. kushoto ni Bibi wa Mtoto huyo Silimagi Manyeji.

Msanii wa Kikundi cha Sanaa cha Ngoma ya Matoigaa Charoo cha Ukara Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza Goabth Bwere akionesha Umahiri  wake katika uwanja wa Bwisye Ukara wakati wa Hafla ya  kuweka Jiwe la Uzinduzi wa Majengo mapya ya Kituo cha Afya  Bwisya Ukara Ukerewe

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu Hassan, akihutubia Wananchi wa wa Bwisye Ukara Wilayani Ukerewe baada ya kuweka Jiwe la Uzinduzi wa Majengo mapya ya Kituo cha Afya  Bwisya Ukara Ukerewe leo.



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu Hassan, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Msanii wa Kikundi cha Sanaa cha Ngoma ya Matoigaa Charoo cha Ukara Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza Goabth Bwere katika uwanja wa Bwisye Baada ya Makamu wa Rais  kuweka Jiwe la Uzinduzi wa Majengo mapya ya Kituo cha Afya  Bwisya Ukara Ukerewe 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela alipowasili Uwanja wa ndege wa Mwanza  akitokea Kisiwani ukara wilani Ukerewe  Baada ya kuweka Jiwe la Uzinduzi wa Majengo mapya ya Kituo cha Afya  Bwisya Ukara Ukerewe.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.