Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein Awapongeza Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes na Kuwakabidhi Fedha Taslim Wakati wa Hafla ya Chakula Alichowaandalia Ikulu leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Ma;pinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akimkabidhi Fedha Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes Ndg. Hemed Suleiman Moroco, kwa Wachezaji na Viongozi walioshiriki Michuano ya Kombe la Chalenji kwa mwaka 2019 inayofanyika Nchini Uganda.Timu ya Zanzibar haijabahatika kuendelea na michuano hiyo baada ya kutolewa hatua za mwazo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.MheDk. Ali Mohamed Shein, akimpongeza Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes Hemed Suleiman Moroco, wakati wa hafla ya chakula Maalum kilichoandaliwa Ikulu Zanzibar kwa ajili ya kuwapongeza Wachezaji hao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwa na Viongozi wa SMZ wakimsikiliza Kocha Mkuu wa Timu ya Zanzibar Heroes Ndg.Hemed Suleiman Moroco akitowa maelezo na kuwatambulisha Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar wakati wa hafla ya chakula maalum kilichoandaliwa na Rais kwa ajili ya kuwapongeza. kulichofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar. 
Kocha Mkuu wa Timu ya Zanzibar Heroes Ndg.Hemed Suleiman Moroco akitowa maelezo na kuwatambulisha Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar wakati wa hafla ya chakula maalum kilichoandaliwa na Rais kwa ajili ya kuwapongeza. kulichofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Gavu akisoma risala ya pongezi kwa Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes walioshiriki michuano ya Kombe la Chalenji Nchini Uganda mwaka huu 2019, akisoma kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa hafla ya chakula maalum walichoandaliwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
KATIBU Mkuu Wizara ya Michezo Vijana Sanaa na Utamaduni Ndg. Omar Hassan (King) akiwa na baadhi ya Wachezaji na Viongozi wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes, wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein ikisoma kwa niaba na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Gavu, iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar
BAADHI ya Mawaziri wa SMZ wakifuatilia hutuba ya kuwapongeza Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes iliofanyika kwa chakula maalum kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar. na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, kuwapongeza wachezaji  wa Timu ya Taifa ya Zanzibar walioshiriki michuano ya Kombe la Chalenji Nchini Uganda.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes na Washauri wa Rais waliosimama nyumba, waliokaa (kutoka kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi, Jaji Mkuu wa Zanzibar.Mhe Omar Othman Makungu, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi.Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee,Kadhi Mkuu wa Zanzibar.Sheikh Saleh Omar Kabi na Kocha Mkuu wa Zanzibar Heroes Hemed Suleiman Moroco na kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Gavu, Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi,MheMgeni Hassan Juma, Waziri wa Michezo Vijana Sanaa na Utamaduni Mhe.Ali Karume na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.Mhe. Hassan Khatib Hassan.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohammed Shein akiwapongeza Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes baada ya hafla ya chakula cha maalum alichowaandali leo Ikulu Jijini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.