Habari za Punde

Mradi wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar wa Terminal III Ukiendelea na Ujenzi Huo.

Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa akitembelea Mradi wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Terminal III, kuona maendeleo ya ujunzi huo akiwa na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mhe.Dr. Ubwa Sira Mamboya (kulia) na (kushoto) Meneja Mradi wa Serikali Eng. Yasser De Costa. 
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa akimsikiliza Meneja Miradi ya Serikali Eng. Yasser De Costa, wakati wa ziara yake kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar Terminal III,akiwa na Wizari wa Ujenzi Usafirishaji na Mawasiliano Mhe. Dr. Sira Ubwa Mamboya.  
WAZIRI wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji, Dk. Sira Ubwa Mamboya, ambae ndie msimamizi mkuu wa ujenzi wa uwanja wa ndege Taminal III,  akitoa maelezo kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Balozi Mohamed Ramia baada ya kufanya ziara ya kutembelea maeneo ya uwanja huo. 
HARAKATI za ushindiliaji kifusi ukiendelea, gari la sagamawe likishindilia kifusi barabara za kutulia ndege upande wa Terminal III.
MSAFARA wa Waziri wa Fedha na Mipango, Balozi Mohamed Ramia, ukiangalia sehemu za mitari ya kupitishia maji.

MSAFARA wa Waziri wa Fedha na Mipango, Balozi Mohamed Ramia, ukiangalia sehemu za mitari ya kupitishia maji.
 PICHA ZOTE NA ABDALLA OMAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.