Habari za Punde

UFUNGUZI WA KAMPUNI YA AD MARK ZANZIBARNa Khadijja Khamis –Maelezo Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed  amesema kuwepo Kampuni ya Kimataifa  inajojishughulisha na masuala ya afya EDMARK International itawasaidia wananchi kupata fursa ya biashara  na kuwajengea afya bora  .
 Hayo aliyasema wakati akizindua Tawi jipya la Kampuni ya EDMARK INTERNATIONAL  kwa upande wa Zanzibar huko  katika Mtaa wa Kiembe Samaki
Alisema matumizi ya bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo zitawasaidia wananchi kuwaondoshea sumu katika miili yao inayotokana na vyakula,mafuta,pamoja na kuwapunguzia uzito mkubwa na magonjwa sugu.     .
Alisema bidhaa hizo zinawanufaisha wananchi kuepukana na matumizi ya  madawa yenye  kemikali hivyo aliwataka viongozi kutoa takwimu ya wagonjwa waliopata mafanikio kwa matumizi  ya dawa hizo ili kuweza  kuisaidia Serikali .
Aidha aliwataka Viongozi wa Kampuni hiyo kupunguza gharama  ya bidhaa zao ili kumuwezesha Mwananchi mwenye hali duni  kuweza kuzimudu .
Nae Afisa Masoko Msaidizi wa Afrika Mashariki Maylyn Guilermo amesema  Tawi limefunguliwa kwa mwendo wa mafanikio hivyo amewataka wanachama kuongeza bidii za kibiashara  na wasiokuwa wanachama kujiunga na biashara AD Mark  ili waone mafanikio  .
Alisema wanachama waliofanya vizuri katika biashara ya bidhaa hizo walipatiwa zawadi mbali mbali ikiwemo safari za nje ya nchi,  gari na nyumba kwa lengo la kujenga ari ya kimafanikio kwa wengine  .
Kwa Upande wa Meneja Muhamasishaji  kwa Upande wa Zanzibar  Riziki Khamis Mgeni  amewataka wananchi wenye matatizo mbali mbali ya maradhi ikiwemo vidonda vya tumbo maradhi ya mifumba na mengineyo kuzitumia bidhaa hizo kuona mafanikio yake
Aidha alisema kuwa dalili ya magonjwa sugu kwa binaadamu huanzia tumboni ,hii inatokana na kukosa choo kikawaida jambo ambalo hukifanya chakula kilichomo kuoza na kuzalisha bakteria ambao husababisha saratani ya utumbo mpana pamoja na vidonda vya tumbo  .
Alifahamisha uzito mkubwa kwa binaadamu huchangia maradhi mbali mbali ikiwemo ugonjwa wa moyo presha na kuzidi kwa tindikali na mafuta mengi mwilini.
Vile vile aliwataka Wananchi kutumia bidhaa hizo kwa kujikinga na kujenga afya zao ikiwemo watoto  .  
Nae Meneja Mkuu Muandamizi  kutoka Tanzania Bara Fred Joel alifafanua bidhaa ambazo zinazalishwa katika Kampuni hiyo zinatokana na vyakula vya kawaida ambavyo humsaidia mtu  kupata virutubisho  katika  mwili ,kusawazisha tindikali na alkali mwilini .
“Ukitumia bidhaa zetu tunakupa uhakika  wa kupata matokeo kwa Asilimia 100  na  usipopata matokeo  ndani ya siku 90 njoo tutakurudishia pesa zako “alisema Meneja Fred
Hata hivyo Mmoja  kati ya Wanachama wa Kampuni ya  EDMARK International  Rukaiya Abeid Mkaazi wa Kijichi alisema alijiunga na kampuni hiyo kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya vidonda vya tumbo na presha kwa muda wa miezi sita mfululizo,baada ya kuanza kuzitumia bidhaa kwa muda wa miezi miwili maradhi yameweza kupotea .
“Nilikuwa sina raha kwa vidonda dawa zote nimemaliza presha juu juu hadi macho pia yakawa hayaoni vizuri lakini baada ya kutumia bidhaa hizi , hali yangu ikaanza kurudi kidogo kidogo namshukuru Mwenyezi Mungu nimepona “,alisema Rukaiya .
Kampuni  ya Kimataifa  inajojishughulisha na masuala ya Afya EDMARK  International imeanzishwa mwaka 1984  iko  zaidi ya nchi 30 duniani kote na matawi zaidi ya 50  na kwa upande wa Tanzania  ina matawi matatu yaliopo Dar- es-salam,  Mwanza na  Zanzibar .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.