Habari za Punde

MKUU WA TAKWIMU ZA BEI ATOA TAKWIMU ZA BEI ZANZIBAR

Mkuu wa Takwimu za Bei kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Khamis Abdul-rahman Msham akitoa Takwimu za Bei ambapo imeonesha kupanda kutoka Asilimia 4.9 kwa mwezi wa January 2020 hadi asilimia 6.2 February 2020 hafla iliofanyika katika ukumbi wa Mtakwimu Mkuu Mazizizni Zanzibar.
Mchumi mwandamizi Chuo Kikuu cha Taifa SUZA Dk,Estella Ngoma Hassan akijibu maswali yalioulizwa atika hafla ya utoaji wa Takwimu za Bei  ambapo imeonesha kupanda kutoka Asilimia 4.9 kwa mwezi wa January 2020 hadi asilimia 6.2 February 2020 hafla iliofanyika katika ukumbi wa Mtakwimu Mkuu Mazizizni Zanzibar. 
Meneja Uchumi Benki kuu ya Tanzania tawi la Zanzibar Moto Ng'winganele Lugobi akitoa ufafanuzi baadhi ya maswali yalioulizwa katika hafla ya utoaji wa Takwimu za Bei  ambapo imeonesha kupanda kutoka Asilimia 4.9 kwa mwezi wa January 2020 hadi asilimia 6.2 February 2020 hafla iliofanyika katika ukumbi wa Mtakwimu Mkuu Mazizizni Zanzibar.
Picha na Yussuf Simai - Maelezo Zanzibar
Na Mwashungi Tahir   Maelezo Zanzibar.
Imeelezwa kwamba  mfumko wa bei kwa mwaka uloishia February 2020  imeongezeka kufikia asilimia 6.2   ukilinganisha  kwa  mwaka ulioishia January 2020 asilimia 4.9  
Hayo ameyasema Mkuu wa Kitengo cha mfumko wa bei kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali  Khamis Abrahmani Msham wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Mtakwimu Mkuu wa Serikali ilioko Mazizini .
Amesema ongezeko hilo limetokana  na bidhaa mbali mbali zikiwemo  vyakula vilivyoongezeka Mchele wa Mbeya , Unga wa Sembe , mafuta ya dizeli. bidhaa zisizo  kuwa na kilevi na bidhaa nyengine Unga wa Ngano .Samaki  Ndizi Mbichi  Sukari Nyeupe  Ndizi mbivu  na Saruji .

Nae Meneja Uchumi wa Bank KuuTawi la Zanzibar Moto Ng’wingamele Lugobi amesema bei imeongezeka lakini bado upo kwa lengo la Serikali ambapo mvua zikienda vizuri bei zitapungua.
Aidha aliwataka kuondosha wasi wasi kuhusu ongezeko la bei kwani hilo ni ongezeko la kawaida na mvua zikiwa zitakwisha bidhaa zitashuka.
Kwa upande wake  Dr Esklla Ngoma  Hassan Mchumi mwandamizi SUZA  amesema kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha  nchini ndio bei za bidhaa zinapanda ukilinganisha na Nchi nyengine za jirani ikiwemo Uganda.

Vile vile wananchi wamesema hivi sasa hali ya bei imezidi kuwa kubwa hali ambayo inawasababishia kutoweza kumudu kupata mahitaji ya lazima ikiwemo samaki, nyama   bidhaa za nafaka, na baadhi ya bidhaa nyengine na misha yanazidi kupanda.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.