Habari za Punde

Vijana wa Wilaya ya Magharibi "B" Unguja Wapata Elemi ya Corona. "Vijana Taveta wapatiwa Elimu ya COVID 19"

Na. Takdir Suweid -Maelezo Zanzibar.
Wananchi wametakiwa kufuata maelekezo yanayotolewa na Serikali kupitia Waalamu wa Afya ili kuweza kujikinga Virusi vya COVID 19 vinavyosababisha Maradhi ya Corona.
Wito huo umetolewa huko Taveta na Makamo Mwenyekiti wa Kamati ya huduma za jamii katika Baraza la Manispaa Wilaya ya Magharibi ‘’B’’ Thuwaiba Jeni Pandu wakati alipokuwa akizungumza na Vijana kuhusiana na Maradhi hayo.
Amesema kamati ya huduma za Jamii ya Baraza la Manispaa Wilaya ya Magharibi B imeweka Mikakati ya kupambana na Virusi hivyo kwa kufanya ziara  katika Soko la Mwanakwerekwe na Mombasa ili kuweka utaratibu wa kuondosha Msongamano wa Wafanyabiashara na kuhamasisha kuwekwa Vitakasa mikono katika maeneo yanayotoa huduma za kijamii ili Wananchi waweze kujikinga na Virusi vya Corona.
Hivyo iwapo Wananchi hawatounga Mkono mikakati hiyo haitoweza kufanikiwa.
Aidha amesema Wameamua kubandika Matangazo katika maeneo yenye Mikusanyiko ya Watu ili kuhakikisha wanatii S heria na yoyote atakaebainika kwenda kinyume na maelekezo yaliokwa atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kulipa faini ya sh.elfu hamsini.
Nao baadhi ya Wakaazi wa Taveta na maeneo ya jirani wameiomba Serikali kuwachukulia hatua kali Wanaotoa Taarifa za Uzushi juu ya Maradhi hayo na kuzusha Taharuki kwa Wananchi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.