Habari za Punde

Wananchi watakiwa kuyatunza miundo mbinu ya maji ya Zawa

Na Takdir Suweid
Wananchi wametakiwa kuwa waangalifu katika kulinda Miondombinu ya Maji ili kunusuru athari zinazoweza kujitokeza ikiwemo kukosa huduma hiyo.
Wito huo umetolewa na Kaimu Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Amina Abdalla Daudi wakati alipokuwa akizungumza na Zbc kuhusiana na upatikanaji wa huduma hiyo.
Amesema kuna baadhi ya maeneo hasa ya njiani,Bomba za Maji zimefukuka kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha jambo ambalo linaweza kusababisha kuharibika na kupoteza maji mengi.
hivyo ni vyema kutoa taarifa katika Mamlaka hiyo wakati wanapoaana Miondombinu ilioharibika ili iweze kufanyiwa matengenezo kwa haraka.
Aidha amesema Mafundi wa ZAWA wanajitahidi kuyafanyia kazi Matatizo ya Wananchi yanapotokezea licha ya kukabiliwa na changamoto ya wingi ya Watumiaji katika maeneo mbalimbali.
Hata hivyo amewataka Wananchi kutumia Maji kwa uangalifu ili yasiweze kupotea na wengine wapate hudumu hiyo hasa katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.