Habari za Punde

SHIRIKA LA UZIKWASA LATOA MSAADA WA VIFAA TIBA NA KINGA WILAYA YA PANGANI


Mkurugenzi wa Shirika la Uzikwasa Novatus Urassa kushoto akikabidhi  Msaada wa Vifaa Kinga na Vifaa Tiba kwa Uongozi wa wilaya ya Pangani anayefuatia kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange na kulia ni Mkurugenzi wa Halmashsuri ya wilaya ya Pangani Isaya Mbenje.

Na.Assenga Oscar.                                                                                                                            

SHIRIKA la Uzikwasa wilayani Pangani Mkoani Tanga limetoa msaada wa vifaa tiba na kinga uongozi wa wilaya hiyo vyenye thamani ya zaidi ya sh.milioni 42 ikiwa ni mkakati wa kuunga mkono juhudi za serikali kwenye masuala ya Afya na katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Covid 19 kwa kutumia bajeti yao ambayo ilipaswa kutumika kwa jamii kwenye kipindi hicho kwa kuona bora wachangia huduma hizo. 

Vifaa vilivyotolewa shirika hilo kupitia wafadhili wao Irish Aid ni pamoja na Oxygeni Concentration Machines,Oxygeni Cylinders,Pulse Oximeters,Thermo Scanners,Surgical Masks,Fullsuit overalls,Motorized Sprayers,Hand Sanitizers ambazo walikabidhi kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya,Kikosi Kazi cha Corona wilaya,Wakuu wa Idara na wadau wengine wilayani humo.



Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani ambaye alimwakilisha Mkuu wa wilaya hiyo, Mwalimu Hassani Nyange alilishukuru Shirika hilo kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kusaidia kwenye masuala ya Afya wilayani humo ikiwemo kuwa mstari wa mbele kuona namna ya kusaidia harakati za kimaendeleo. 

Mwalim Nyange alisema moja ya maeneo muhimu kwa uzikwasa wameyalangea ni afya na fedha hizo sio ndogo kwenye uwekezaji wa afya kwani wangeweza kuzitumia kwenye matumizi mengine lakini wao wakaona wanunue vifaa kwa ajili ya kutoa mchango wao kwenye mapambando dhidi ya Covid 19. 

“Wote tunajua Corona bado ipo na tuendelee kuchukua tahadhari hivyo msaada huo ambao umetolewa na Shirika hili ni muhimu na umefika wakati muafakA tunapo pambana janga hilo na kuchukua hatua ambavyo tumeelekezwa na wataalamu wa afya hapa nchini “Alisema 

Aidha alisema Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli imekuwa makini sana kwenye masuala ya Afya kwani miaka ya nyuma kulikuwa na tatizo kubwa la dawa hospitalini hata watumishi wasiokuwa waaminifu walikuwa wanaanzisha maduka yao lakini leo baada ya bajeti ya dawa kuongezeka imesaidia sana kuondosha changamoto hizo 

Katibu Tawala huyo alisema kwenye awamu hiyo serikali imewekeza sana kwenye huduma za Afya kwa kujenga hospitali za wilaya, vituo vya afya, kikanda kimkakati yote ni jitahada ya serikali ya awamu ya tano na wizara ya afya ambao wamefanya kazi kubwa kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora wanapofika kwenye maeneo husika. 

Hata hivyo katibu Tawala huyo aliwataka wahudumu wa afya washukeni kwenye ngazi za shule za msingi na sekondari ili kuweza kuwapa hamasa wanafunzi kuwa na hamu ya kusoma masomo ya sayansi ili kuweza kupatikana wataalamu wengi ambao watakuwa chachu katika sekta hiyo muhimu hapa nchini 

“Binafsi hata mimi nimekuwa nikifanya hivyo kwenye maeneo ya shule za Sekondari na kwenye mikutano lakini tutambue uzalendo unarisidhwa kuanzia chini kabla ubongo wao haujaingiliana na mambo mengi kwani watoto wengi wanaotaka kusoma masomo hayo wanapotea kuanzia ngazi ya chini”Alisema Mwalimu Nyange. 

Awali akizungumza katika halfa ya makabidhiano hayo Mkurugenzi wa Shirika la Uzikwasa Novatus Urassa alisema kwa kutambua umuhimu wa jamii wanayoihudumia pamoja na ushirikiano mzuri kati yao na wadau wengine wilayani humo waliona ni vyema kuongeza juhudi kwenye suala la afya na mapambano dhidi ya Corona. 

Alisema kwamba kwa kutumia bajeti ambayo ilipaswa kutumika kwa jamii kipindi hiki walionelea ni vizuri waweze kuchangia huduma za afya kwenye vifaa kinga na vifaa tiba huku wakiwashukuru wafadhili wao Irish Aid kuwaruhusu waweze kubadili matumizi ya bajeti ya shughuli zao kuwezesha kununua vifaa hivyo. 

“Vifaa hivi ambavyo tunavikabidhi leo hii vitatumika katika hospitali ya wilaya ya Pangani, Kituo cha Afya Mwera, Zahanati ya Kipumbwi na Mkalamo ambacho ni kituo cha Afya tarajiwa”Alisema Mkurugenzi huyo. 

Awali akizungumza katika halfa hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Pangani Isaya Mbenje alisema wao walikuwa wanawasiliana na wadau mbalimbali kuona namna ya kuwasaidia vifaa vya afya na ambavyo vitatumika kwenye mapambano dhidi ya Covid 19 na waliweza kuwasiliana na Shirika la Uzikwasa. 

Alisema baada ya kuwasiliana nao wakaonyesha nia ya kuweza kuwasaidia na walimpigia simu kumueleza namna walivyofanikiwa kupatikana vifaa hivyo ambayo waliwakabidhi kwa ajili ya ugawaji kwenye maeneo mbalimbali kwenye wilaya hiyo 

“Niwashukuru Uzikwasa na timu yake kwa kazi kubwa mnayoifanya kusaidia jamii ya watu wa Pangani…vifaa hivi vitasaidia kuimarisha utoaji wa huduma za afya katika wilaya ya Pangani lakini kubwa zaidi nimeambiwa vimenunuliwa katika mfumo wa serikali maana vimepatika kutoka Bohari ya Dawa (MSD)na vimehakikiwa na kukidhi ubora wa kuweza kutumia na kutoa hduma kwa wananchi”Alisema Mkurugenzi huyo.
Mkurugenzi wa Shirika la Uzikwasa Novatus Urassa kushoto akikabidhi  Msaada wa Vifaa Kinga na Vifaa Tiba kwa Uongozi wa wilaya ya Pangani anayefuatia kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange.
KATIBU Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalim Hassani Nyange akizungumza kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Isaya Mbenje na kushoto ni Mkurugenzi wa Uzikwasa Novatus Urassa
Mkurugenzi wa Uzikwasa Novatus Urassa akizungumza wakati wa halfa hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Isaya Mbenje akizungumza wakati wa halfa hiyo kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange na Mkurugenzi wa Uzikwasa Novatus Urassa.
Katibu Tawala wa wilaya Pangani Mwalimu Hassani Nyange katika akiwa kwenye picha ya pamoja kushoto ni Mkurugenzi wa Uzikwasa Novatus Urassa na kulia ni Mkurugenzi wa Halamshauri ya wilaya ya Pangani Isaya Mbenje na Mkuu wa Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina Matagi

 Sehemu ya vifaa vilivyotolewa.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.