Habari za Punde

MHADHIRI WA CHUO KIKUU APATA AJALI AKIENDA KUCHUKUA FOMU JIMBO LA SIHA

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria ,Kulwa Mang'ana akiwa nje ya gari lake muda mfupi baada ya kupata ajali akiwa njiani akiwa njiani kuelekea Siha kwa ajili ya kuchukua fomu za kugombea nafasi ya Ubunge katika jimbo la Siha .

Na Dixon Busagaga,Hai 
Mhadhiri wa Chuo Kikuu huria Tanzania, Kulwa Mang'ana amepata ajali katika eneo la Boman'gombe wilayani Hai wakati akiwa njiani kuelekea Wilaya ya Siha kwa lengo la kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ilitokea majira ya saa 10:00 jioni njia panda ya kuelekea Siha ambapo dereva wa pikipiki aliigonga gari yake kwenye eneo la mlango wa dereva na kusababisha kuvunjika kwa kioo ambacho vipande vyake vilimuingia sehemu za mwili ikiwemo kichwani.

Baada ya taratibu za kisheria kukamilika katika kituo Cha Polisi Cha Bomang'ombe ,Ndugu Kulwa alieleza kusitisha zoezi la kwenda kuchukua fomu huku akiwatakia kila la kheri wote waliojitokeza kuchukua fomu katika Jimbo hilo wakiwemo Aggrey Mwandry na Dkt Godwin Mollel.

Hivyo ameachana na dhamira hio kwa kuwa baadhi ya  viongozi  hawa wamewatumikia wananchi vyema na kuaminiwa na  raisi wetu John Pombe magufuli, nae ameona wanatosha kabisa. Amesema atasubiri mpaka 2025 kwa sasa ataendelea kuwa mwanachama mtii,muaminifu na mzalendo kwa nchi yake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.