Na.Jaala Ali ZEC.
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imemtangaza rasmin Mgombea wa Uwakilishi kwa tiketi ya Chama cha
Mapinduzi Mhe. Haji Omar Kheir kuwa Muwakilishi mteule wa Jimbo la Tumbatu.
Msimamizi wa Uchaguzi ZEC
Wilaya ya Kaskazini “A” Bi.Miza Pandu Ali akizungumza na Vyombo vya habari katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar zilizoko Gamba amesema Tume imetoa Uamuzi wa Kumtangaza Mgombea huyo baada ya kuwa ni Mgombea pekee wa nafasi ya Uwakilishi kwa Jimbo la Tumbatu Zanzibar.
Msimamizi huyo alieleza kuwa Tume imefanya maamuzi kwa mujibu wa masharti ya Sheria ya Uchaguzi ya
Zanzibar Nam. 4 ya 2018 kifungu cha 59(a)(b)
ambacho kinamtaka msimamizi wa Uchaguzi kumtangaza Mgombea pekee katika Jimbo au Wadi.
Aidha, Tume imemtangaza Ndg.Othman
Khamis Fumu kuwa Diwani Mteule wa Wadi ya Kipange na Ndg.Simai Vuai Khamis kuwa Diwani Mteule wa Wadi ya Kijini kwa tiketi ya
Chama cha Mapinduzi.
Akizungumza kwa niaba ya wateule wenzake Mhe.
Haji Omar Kheir alisema Wagombea wote katika jimbo la Tumbatu wameridhishwa na busara na hekima kwa Watendaji wa Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar katika kufanya maamuzi sahihi ya pingamizi na rufaa zilizowasilishwa.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari juu ya uamuzi wa Rufaa iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi ilimuengua Ndg.Haji
Ali Haji Mgombea wa nafasi ya uwakikishi Jimbo la Tumbatu Zanzibar , Zuli Juma Simba Wadi ya Kijini na Salum Khamis
Maliki Wadi ya Kipange wote kwa tiketi ya ACT Wazalendo baada ya kushindwa kutimiza vigezo vya uteuzi.
No comments:
Post a Comment