Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Atembelea Hospital ya Micheweni Pemba.

MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla, akipata maelezo juu ya ufanyaji kazi wa mashine ya X-Ray kutoka kwa Dk Ali Khamis, wakati alipofanya ziara ya kutembelea hospitali ya Micheweni, wakati wa ziara yake ya siku tatu Kisiwani Pemba.
MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla, akimsikiliza mmoja ya wafanyakazi wa chumba cha Upasuaji katika Hospitali ya Micheweni, juu ya kudai fedha zao za muda wa zaira kwa muda wa miaka miwili na nusu sasa hawajalipwa na uongozi wa Wizara ya afya, wakati wa ziara yake ya siku tatu Kisiwani Pemba
DAKTARI dhamana wa Hospitali ya Micheweni Dk Mbwana Shoka Salim, akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla, juu ya ufanyajai kazi wa mashine ya kuchomea takataka katika hospitali ya Micheweni, , wakati wa ziara yake ya siku tatu Kisiwani Pemba
MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdalla, akizungumza na watendaji wa Wizara ya afya na uongozi wa Hospitali ya Micheweni, baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua maendeleo ya hospitali hiyo, , wakati wa ziara yake ya siku tatu Kisiwani Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.