Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMUWAKLILISHA RAIS DKT. MAGUFULI KWENYE MKUTANO WA DHARURA WA SADC, ORGAN TROIKA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Rais Felix Antoine Tshisekedi wa Congo DRC na Rais wa Emmerason Mnangagwa wa Zimbabwe baada ya kumalizika kwa mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa dharura wa pamoja baina ya SADC, ORGAN TROIKA, Nchi zinazochangia Vikosi vya Ulinzi na Amani vya Umoja wa Mataifa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo  kwenye Kikosi cha Umoja wa Mataifa DRC, uliojadili kuhusu hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika na kuweza kuona changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika eneo la Siasa, Ulinzi na Usalama ili kwa pamoja kuweza kupata utatuzi wa mambo yatakayobainishwa katika mkutano huo uliomalizika leo Jijini Gaborone Nchini Botswana. kwenye mkutano huo Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Ujumbe wa Tanzania  kwenye mkutano wa dharura wa pamoja baina ya SADC, ORGAN TROIKA  Nchi zinazochangia Vikosi vya Ulinzi na Amani vya Umoja wa Mataifa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwenye Kikosi cha Umoja wa Mataifa DRC, unaojadili kuhusu hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika na kuweza kuona changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika eneo la Siasa, Ulinzi na Usalama ili kwa pamoja kuweza kupata utatuzi wa mambo yatakayobainishwa katika mkutano huo uliomalizika leo Novemba 27,2020 Jijini Gaborone Nchini Botswana. kwenye mkutano huo Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

 (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.