Habari za Punde

Kaimu Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii Jinsia na Watoto awataka watendaji Ofisi za Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi (ZFDA) kuwa na ushirikiano mzuri

Kaimu Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii Jinsia na Watoto ambae pia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said alipokuwa akizungumza na watendaji wa ofisi za wakala wa chakula, dawa na vipodozi (ZFDA) alipofanya ziara ya kushtukiza hapo jana.
Kaimu Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii Jinsia na Watoto ambae pia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akimsikiliza mmoja watendaji wa ofisi za wakala wa chakula, dawa na vipodozi (ZFDA) alipofanya ziara ya kushtukiza hapo jana.

Kaimu Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii Jinsia na Watoto ambae pia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akitoa maelekezo kwa watendaji wa wa ofisi za wakala wa chakula, dawa na vipodozi (ZFDA) alipofanya ziara ya kushtukiza hapo jana.

Picha na Maulid Yussuf , Wema


Na Maulid Yussuf, Wema


 Kuwepo kwa bidhaa bora na zenye Kiwango imara kutaipelekea Taifa kuwa na jamii yenye Afya imara ambao ndio tegemeo kuwa viogozi WA baadae.

Kaimu Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii Jinsia na Watoto ambae pia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za wakala wa chakula, dawa na vipodozi (ZFDA), na kukagua shughuli mbalimbali zilizopo chini ya ofisi hiyo huko Mombasa mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Amesema ili jamii ihakikishe inatumia bidhaa bora ni lazima wakala hao kuhakikisha kuwa bidhaa zinazoingia nchini, zinafanyiwa ukaguzi kabla ya matumizi ya mwanaadamu.
Aidha mhe Said amewataka watendaji wa wakala wa chakula, dawa na vipodozi ZFDA kuwa na ushirikiano mzuri katika kazi ili kuendelea kuimarisha huduma za upatikanaji wa bidhaa zinazoingia na ziliopo nchini kuwa kwenye Kiwango kizuri kwa ajili ya matumizi ya binadamu.
Kwa upande wao watendaji wa Wakala wa Chakula, dawa na vipodozi ZFDA, wamemshukuru Mhe Simai kwa uamuzi aliouchukua kufika katika ofisi zao kwa lengo la kuona utendaji kazi kwa mamlaka yao, jambo linaloashiria ushirikiano wa karibu baina ya viongozi na watendaji wa chini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.