Habari za Punde

Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Kaskazini Unguja akabidhi msaada wa vifaa Hospital ya KivungeMkurugenzi Tiba  Wizara Ya Afya Juma Salum Mbwana akizungumza machache na kumkaribisha Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Sada Mansur kukabidhi vifaa mbali mbali vya matumizi ya Hospitali hafla iliyofanyika Hospital ya Wilaya Kivunge Zanzibar .

Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Sada Mansur akizungumza machache kabla ya kukabidhi  vifaa mbali mbali vya matumizi ya Hospitali hafla iliyofanyika Hospital ya Wilaya Kivunge Zanzibar.

Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Sada Mansur akimkabidhi  Mkurugenzi Tiba  Wizara Ya Afya Juma Salum Mbwana televisheni kwaajili ya watu wanaofika hospitalini hapo kukaa na wagonjwa wao  hafla iliyofanyika Hospitali ya Wilaya Kivunge Zanzibar.


Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Sada Mansur akimkabidhi  Mkurugenzi Tiba  Wizara Ya Afya Juma Salum Mbwana kitanda cha mazoezi kwa ajili ya wagonjwa huko  Hospitali ya Wilaya Kivunge Zanzibar. . 

Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Sada Mansur akimkabidhi  Mkurugenzi Tiba  Wizara Ya Afya Juma Salum Mbwana kitanda  na godoro kwa ajili ya wagonjwa ambao watalazwa katika jengo la mama na mtoto  huko  Hospitali ya Wilaya Kivunge Zanzibar.   
Mkurugenzi Tiba  Wizara Ya Afya Juma Salum Mbwana aahidi kuvitunza vifaa vilivyotolewa msaada na  Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Sada Mansur na kuvitumia ipaswavyo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika Hospital ya Wilaya Kivunge Zanzibar.   
Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Sada Mansur akisoma taarifa fupi ianyohusiana na vifaa mbali mbali alivyomkabidhi  Mkurugenzi Tiba  Wizara Ya Afya Juma Salum Mbwana huko  Hospitali ya Wilaya Kivunge Zanzibar. 
Mganga Mkuu Msaidizi Hospitali ya Wilaya Kivunge Juma Ali Makame akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wafanyakazi wa Hospitali ya Wilaya Kivunge jengo la mama na mtoto mara baada ya kupokea msaada wa vifaa vya matumizi ya hospitali kutoka kwa  Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Sada Mansur 
Mganga Mkuu Msaidizi Hospitali ya Wilaya Kivunge Juma Ali Makame akimtembeza  Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Sada Mansur maeneo mbalimbali ya jengo la mama na mtoto huko  Hospitali ya Wilaya Kivunge,ikiwemo chumba cha upasuaji kwa mama wajawazito .
 Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Sada Mansur akiwajuulia hali mama mbalimbali ambao walifika hospital ya Wilaya Kivunge  kwa ajili ya kupata huduma ya kujifungua .Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Sada Mansur akisikiliza maelekezo kutoka kwa  Mkurugenzi Tiba  Wizara Ya Afya Juma Salum Mbwana  wakati alipokuwa akitembelea wodi mbali mbali katika jengo la mama na mtoto huko Hospital ya Wilaya Kivunge Zanzibar.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.