STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar
07.12.2020
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Hussein Ali Mwinyi amewateua Nassor Ahmed Mazrui na Omar Said Shaaban.
Kwa mujibu wa taarifa
kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu
Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, ilieleza kwamba uteuzi huo umeanza leo
tarehe 7 Disemba, 2020.
Aidha, taarifa hiyo
ilieleza kwamba kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 66 cha
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi amewateua viongozi hao kuwa Wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment