Habari za Punde

Waziri wa Mambo ya Nje wa China kuwasili Nchini Kesho

Na. Immaculate Makilika- MAELEZO, Chato

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wangi Yi anatarajiwa kuwasili nchini kesho Januari 7, 20201 katika Uwanja wa Ndege wa Geita uliopo Wilaya ya Chato kwa ajili ya kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Chato mkoani Geita, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi alisema kuwa Waziri Yi atakapokuwa nchini atafanya shughuli mbalimbali ikiwemo uzinduzi wa Chuo cha Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA) cha Wilaya ya Chato mkoani Geita.

“Hapo kesho mara baada ya kuwasili hapa Chato, Waziri Yi atazindua Chuo cha VETA cha Wilaya ya Chato ambacho kimejengwa kwa fedha za watanzania na Ukumbi mmoja ambapo umepewa jina lake” alisema Prof. Kabudi.

Alisisitiza: “Sababu ya kumuomba afungue chuo hicho ni utamaduni wetu wa kumpa heshima mgeni anapokuja hapa kwetu, sambamba na kutambua elimu ya mafunzo na ufundi stadi ilivyopiga hatua huko nchini China.”

Prof. Kabudi aliongeza kuwa Serikali ya China inatarajia kujenga Chuo cha Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA) mkoani Kagera ikiwa ni namna ya kufikia lengo la Serikali  ya Awamu ya Tano ya kujenga VETA kila wilaya hapa nchini.

Alitaja shughuli zingine zitakazofanywa na Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa China, kuwa ni mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, pamoja na kufanya  mazungumzo rasmi kati yake na ujumbe wake kutoka nchini China.

Aidha, masuala mengine ambayo Mawaziri hao wa Mambo ya Nje watayazungumza ni pamoja na kupanua wigo wa biashara za Tanzania nchini China, kushiriki maonesho ya biashara ili kukuza bidhaa za Tanzania pamoja uwekezaji katika sekta ya madini.

Utoaji wa mikopo nafuu katika uzalishaji wa umeme wa maji katika baadhi ya maeneo nchini. Shughuli nyingine atakazofanya Waziri Yi ni pamoja na kutembelea mwalo wa Chato ili kuona shughuli za uvuvi, ikizingatiwa kuwa Ziwa Viktoria ni Ziwa la pili kwa ukubwa dunia.

Fauka ya hayo, Mawaziri hao watashugudia mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha tano kutoka Mwanza hadi Isaka kitakachogharimi shilingi trilioni 3.0617.

Vilevile, Prof. Kabudi alisema kuwa ziara hii imesaidia kuwataarifu watu wa China kuhusu hifadhi tano mpya ikiwemo ya Burigi-Chato. Ambapo

mwezi Februali mwaka huu Serikali inatarajia kuanzisha  safari za ndege za moja kwa moja kutoka Dar es salaam hadi Guanzhou  nchini China ili kukuza biashara na sekta ya utalii. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.