Habari za Punde

Baraza la Taifa la Ushauri kwa Watu Wenye Ulemavu Wakutana na Kujadili Masuala Mbalimbali Kuhusu Watu Wenye Ulemavu.

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Ushauri kwa Watu wenye Ulemavu Dkt. Lukas Kija (kushoto) akizungumza na wajumbe wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha kwa ajili ya kujadili masula mbalimbali ya Watu wenye Ulemavu. Kulia ni Bi. Christina Mero mjumbe wa Baraza hilo.
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Watu wenye Ulemavu ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Taifa la Ushauri kwa Watu wenye Ulemavu Bw. Jacob Mwinula akieleza jambo wakati wa kikao kazi hicho kazi kilichowakutanisha kwa ajili ya kujadili masula mbalimbali ya Watu wenye Ulemavu.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Taifa la Ushauri kwa Watu wenye Ulemavu wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakiwasilishwa na Katibu wa Baraza hilo (hayupo pichani). Wa pili kutoka kushoto ni Mkalimani wa Lugha ya alama Bw. Adrian Chiyenje.

Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Taifa la Ushauri kwa Watu wenye Ulemavu wakipitia taarifa wakati wa kikao kazi hicho kilichowakutanisha kwa ajili ya kujadili masula mbalimbali ya Watu wenye Ulemavu.

 Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu 

(Kazi, Vijana, Ajira na Wwenye Ulemavu )

OWM - KVAU

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.