Habari za Punde

UVCCM Wilayani Handeni Yawaenzi Wahanga wa Mafuriko Siku ya Siku ya Maadhimisho ya Miaka 44 ya CCM

Na Hamida Kamchalla, HANDENI.

MWENYEKIT wa Umoja wa Vijana wa Ccm wilayani Handeni Ahmadi Chihumpu amewataka vijana wilayani humo kuacha tabia ya kukaa vijiweni na kukiingiza kwenye makundi mabaya badala yake wafanye kazi halali ili kukuza kipato na kuendelea kudumisha amani.

Chihumpu alitoa wito huo mwishoni mwa wiki katika kata ya Kwediyamba  wakati wa kilele cha kuazimisha miaka 44 ya Ccm ambapo Umoja huo uliweka kambi yake na kumalizia sherehe hizo kwa kuwakumbuka wahanga wa mafuriko na kuwapelekea misaada ya kwa ajili ua wanafunzi. 

Alieleza kwamba ili kujenga Taifa la vijana wenye nguvu na imara hawana budi kkufanya kazi kwa bidii na utii na kuacha kukaa vijiweni wakitumia vilevi ambavyo husababisha kuua nguvu ya Taifa huku akiongeza kusisitiza kwamba wanatakiwa kuilinda amani na kuwalinda viongozi, wazee pamoja na akina mama na watoto na kuwa na nchi ya mfano.

"Sisi umoja wa vijan wilaya ya Handeni tumeamua kuja kata hii ya Kwediyamba kufanya majumuishi ya sherehe hii ya chama na tumewatembelea wahanga waliokumbwa na janga la mvua lakini piq tumewaletea msaada huu mdogo wa vifaa vya shile ambavyo vitawasaidia wanafunzi, napenda kuwaasa vijan wenzangu waachane na makundi mabaya na kujiunga kwa pamoja tufanye kazi na kujiletea kipato" alisema Chihumpu.

"Tukifanya kazi kwa bidii naamini hakuna kijana atakayetetereka katika maisha na tutaishi kwa kujiamini bila kupitia njia za panya, hapa namaanisha utakapofanya kazi yako kwa kujiamini utaepukana pi na suala zima la rushwa, niwaombeni tuendelee kuwalinda viongozi wetu wa chama, wazee wetu na pia wakina mama na watoto ili tuendelee kudumu katika amani yetu" aliongeza.

Sambamba na hayo Chihumpu aliwapongeza na kuwashukuru wabunge wa majimbo ya Handeni mjini Reuben Kwagilwa kuwa mstari wa mbele na kuwafikia wananchi wake mara tu wapatapo majanga huku mbunge wa vijijini John Sallu kwa kukabidhi miti ipatayo elfu tatu kwa wananchi wake ili kuzuia ukame katika baadhi ya maeneo wilayani humo.

Kwa upande wa wananchi wa kata hiyo wameelezea furaha yao na kutoa pongezi kwa mbunge wao pamoja na umoja wa vijana kwa kuwajali na kuwapelekea misaada na kuongeza kuwa hawakuwahi kufikiriq kuhusu umoja huo kama unaweza kuwafanyia makubwa na kuwarudishia amani ambayo wengi wao walianza kukata tamaa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.