Habari za Punde

UWT Yawata Wanawake Kujenga Tabia ya Kupima Afya Zao, Agenda ya Lishe Kuwekwa Kwenye Kila Kikao cha CCM.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania Wiaya ya Bukoba mjini Bi Anna Kajuna akishiriki zoezi la  upimaji wa afya  katika kituo cha afya Zamuzamu wakati  wa sherehe za maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa  kwa Chama Cha  Mapiduzi 
Katibu wa jumuiya ya umoja wa wanawake wa Tanzania UWT Mkoa wa Kagera aliyeshika box la sabuni akikabidhi mche wa sabuni kama zawadi kwa mmoja wa wakina mama aliyejifungua katika wodi ya wazazi kituo cha  afya Zamuzamu wakati  wa sherehe za maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa  kwa Chama Cha  Mapiduzi.
Katibu mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Hamimu Mahamudu akiwahutubia wakina mama wakati  wa sherehe za maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa  kwa Chama Cha  Mapiduzi Februari 01,2021 katika kituo cha afya Zamuzamu Bukoba mjini.
Bi Dunia mtaalamu wa afya katika  kituo cha afya Zamuzamu akitoa elimu ya ugonjwa wa salatani ya mlango wa kizazi kwa wanawake waliojitokeza wakati  wa sherehe za maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa  kwa Chama Cha  Mapiduzi

Picha ya pamoja ya viongozi wa UWT mkoa na wilaya ya Bukoba, Mgeni  Rasmi Ndg. Hamimu Mahamudu alishika ilani na kunyoosha mkono, watumishi wa kituo cha afya Zamuzamu na wanawake wa jumuiya ya UWT wakati  wa sherehe za maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa  kwa Chama Cha  Mapiduzi Februari 01,2021.

Na Allawi Kaboyo – Bukoba.

Umoja wa wanawake Tanzania Mkoa wa Kagera katika kuadhimisha miaka 44 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamefanya mambo mbalimbali ndani ya Manispaa ya Bukoba ikiwemo kupatiwa elimu ya afya kuhusu salatani ya mlango wa kizazi pamoja na lishe bora.

Warsha hiyo imefanyika kaika viwanja vya kituo cha afya Zamuzamu kilichopo kata ya Bilele feburuari 01,mwaka huu, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa jumuiya hiyo wa mkoa na wilaya huku mgeni rasmi akiwa ni katibu mwenezi wa chama hicho Ndg. Hamimu Mahamudu.

Akitoa elimu kwa wanawake waliohudhuria warsha hiyo kuhusu salatani ya mlango wa kizazi Bi Dunia ameeleza kuwa watu walio hatalini kuambukizwa au kupata ugonjwa huu ni wasichana walioanza kufanya ngono kwa umri mdogo, mwanamke mwenye wanaume wengi kwa wakati mmoja, mwanamke anayevuta sigara na mwanamke mwenye maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Dunia ameongeza kuwa salatani hiyo inatibika hivyo wanawake wanatakiwa kujenga tabia ya kupima mara kwa mara kwa kuwa dalili zake hazionekani haraka japo madhara yake ni makubwa pale inapochelewa kutibiwa.

Kwaupande wake mtaalamu wa lishe kwaniaba ya afisa lishe manispaa ya bukoba amesema kuwa watoto wengi wamekuwa wakizaliwa wakiwa na matatizo mbalimbali yakiwemo ya udumavu, lishe duni kutokana na mama zao kutozingatia mlo kamili.

Ameonngeza kuwa tatizo la udumavu na lishe duni kwa  watoto limekuwa sugu  hasa kwa ukandaa huu  wa Kagera hali inayopelekea kuwepo kwa namba kubwa ya watoto wenye udumavu na kuwashauri wanawake kuzingatia aina za vyakula wanavyotakiwa kula wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua ili kumjengea mtoto afya njema.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo katibu mwenezi wa ccm Kagera Hamimu Mahamudu ameishukuru jumuiya hiyo kwa kuadhimisha kuzaliwa kwa chama chama chao kwa kuwapa wanawake elimu hasa inayo husu afya ya mama na motto maana kundi hilo ndilo linalotegemewa.

Amewataka wanawake waliopata elimu hiyo kuwa mabalozi wema kwa wanawake wengine kwa kuwapa elimu waliyoipata huku akiagiza vikao vyote vya chama hicho kwa ngazi zote kuweka agenda ya lishe.

“Ninakushukuru mwenyeki wa UWT kwa jambo hili, huwezi kuwaongoza wanachama au wananchi wakiwa hawana afya, kwa mantiki hiyo kama msemaji wa chama wa Mkoa huu naagiza kwenye vikao vyenu na vya chama kuanzia ngazi ya shina hadi mkoa kuwepo na agenda ya lishe” Amesema Mahamudu.

Hamimu ameupongeza uongozi wa kituo cha afya Zamuzamu kwa  usimamizi mzuri  ambao umepelekea kituo hicho kuboreshwa na kuwa na wodi kubwa ya wazazi, chumba cha upasuaji, maabara ya kisasa na miundombinu iliyoimara huku kikiongeza idadi ya wattumishi kutoka watumishi 28 hadi 51 waliopo sasa.

Bi Anna Kajuna ni  mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Bukoba mjini ambaye ameeleza mambo waliyoyafanya kituoni hapo ikiwemo elimu ya afya, upimaji wa salatani ya mlango wa kizazi, utoaji wa damu na ukaguzi wa miundombinu ya kituo hicho.

Mama Kajuna amewataka wanawake kuzingatia elimu waliyopata huku akiwataka kujenga tabia ya kupima afya hali itakayowapelekea kuzitambua afya zao  pamoja na kuanza matibabu maramoja pale watakapogundulika na magonjwa mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.