Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi Ahudhuria Hafla ya Kitaifa ya Kuuaga Mwili wa Hayati John Pombe Magufuli Kitaifa Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma leo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwasili katika Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma kuhudhuria hafla ya Kitaifa ya kuuaga mwili wa Hayati John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman alipowasili katika jukwaa la Viongozi katika Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma kuhudhuria hafla ya Kitaifa ya kuuaga mwili wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
MAKAMANDA wa Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ  wakiwa wamebeka jeneza la mwili wa Hayati John Pombe Magufuli wakiwa katika Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma  wakiupeleka katika eneo maalum lililoandaliwa kwa ajili ya kuuaga Kitaifa. 
MAKAMANDA wa Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ  wakiwa wamebeka jeneza la mwili wa Hayati John Pombe Magufuli wakiwa katika Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma  wakiupeleka katika eneo maalum lililoandaliwa kwa ajili ya kuuaga Kitaifa 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi akitowa salamu za mwisho za heshima kwa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Kitaifa katika Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akitowa salamu za mwisho kwa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya Kitaifa ya kuuaga Mwili wa marehemu iliofanyika katika Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma 
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Venance Mabeyo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi wakiwa wamesimama wakati Mwili wa Hayati Dkt.John Pombe Magufuli ukiwasili katika Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma kwa ajil ya Hafla ya Kitaifa ya kumuaga marehemu 
MJANE wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Mama Janeth Magifuli akitowa heshima za mwisho kwa Marehemu wakati wa hafla ya Kitaifa ya kuuaga mwili wa marehemu katika Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma.
RAIS wa Jamuhuri ya Watu wa Comoro Mhe. Azali Asoumani na Mkewe wakitowa heshima za mwisho kwa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa hafla ya Kitaifa ya kumuaga marehemu katika Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.