Habari za Punde

Wanachama wa CCM Watakiwa Kulipia Ada za Chama Ili Kiweze Kuimarika Zaidi.

Na Mwashungi Tahir     Maelezo     15./3/2021.

MLEZI wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya WAZAZI Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa DK. Edmund Mndolwa  amewahimiza wanachama kulipa ada ya  Chama ili kiweze kuimarika zaidi.

Ameyasema hayo huko katika ukumbi wa Mkoa wa Amani wakati alipokuwa  katika mkutano na wanachama wa CCM na jumuiya zake ikiwemo vijana, wazazi na UWT pamoja  na mabalozi kwa lengo la kuwapongeza kwa ushindi mkubwa uliopatikana kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika 2020.

Amesema  ili chama kiweze kuimarika ni lazima wawe mstari wa mbele katika kulipa ada kila mwaka na sio kusubiri wakati wa uchaguzi kwani kufanya hivyo haipendezi.

Aidha mlezi huyo amewaasa wanachama na jumuiya zake kujiepuha na makundi kwani yanaathiri maendeleo ya chama na kuondoa upendo na badala yake kuwekeana chuki ambapo jambo hilo haliwezi kuleta maendeleo.

Pia amewataka vijana kukilinda chama na kuacha kutumiliwa kwa njia ambayo itakiharibia chama cha Mapinduzi katika kufanya kazi zake kwani kazi nyengine ya kukipatia ushindi bado inahitajika baada ya miaka mitano ijayo 2025.

Mlezi Edmund amempongeza Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi kwa  kushinda kwa kishindo na kuuombea kwa Mungu yale yote aliyoyatarajia kuyafanya Mungu ampe nguvu.

Nae Katibu wa CCM  Mkoa wa Mjini Kichama  Abdullah Mwinyi amesema kazi kubwa ya chama inafanywa na mabalozi hivyo anaomba wapatiwe posho ili waweze kujikimu kimaisha wao pamoja na familia zao.

Akitoa neno la shukurani Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Mgeni Juma amemshukuru mlezi huyo kuja kuwapongeza wananchama na kumuomba kuwaombea akinamama kuongezewa nafasi za viti maalum ili sauti zao ziweze kusikika zaidi na kuletea maendeleo ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.