Habari za Punde

Madaktari Watakiwa Kutowa Elimu Kwa Jamii Ili Kuepesha Maradhi Yasioambukiza.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho Tanzania  Kazim Akbar Dhalla akitoa mafunzo kwa madaktari wa Zanzibar kuhusu upofu wa macho unaosababishwa na maradhi yasioambukizwa huko Hospitali kuu ya Mnazimmoja, mafunzo hayo yatatolewa kwa  muda wa siku tatu kuanzia tarehe 23 hadi 25 mwezi huu.

 Dkt Salama Asaa Ali akichangia mada baada ya kupata mafunzo kuhusu upofu wa macho unaosababishwa na maradhi yasiyoambukizwa kutoka kwa Bingwa wa Magonjwa ya Macho Tanzania  Kazim Akbar Dhalla huko Hospitali kuu y a Mnazimmoja mafunzo hayo yatatolewa kwa  muda wa siku tatu kuanzia tarehe 23 hadi 25 mwezi huu.

 Picha na Bahati Habibu -- Maelezo.

Na Khadija Khamis – Maelezo .23/06/2021.

Daktari Bingwa wa Macho Tanzania  Dk.Kazim Akber Dhalla amewataka madaktari kutoa elimu ya kutosha kwa jamii ili kuepukana na maradhi yasioambukiza ikiwemo presha na sukari ambayo huchangia kwa kiasi kikubwa Kupoteza upofu wa macho.

Alisema tafiti zinaonyesha tatizo la macho ni kubwa zaidi kwa Zanzibar kuliko Tanzania Bara  jambo ambalo linahitaji elimu kubwa kwa jamii.

Hayo aliyasema huko Hospitali ya Rufaa Mnazi mmoja Jijini Zanzibar wakati akitoa mafunzo kwa Madaktari mbali mbali wanaoshughulikia maradhi yasiyo ambukiza ikiwemo presha sukari na macho.

Tafiti iliofanyika Mkoani Kilimanjaro zimeonyesha Wagonjwa waliofanyiwa vipimo ni 3,463 wasiona ni asilimia 4.2 wenye matatizo ya macho ni asilimia 9.2 kwa upande wa Zanzibar waliopatiwa vipimo katika Hospitali kuu Mnazi mmoja ni 356 wasiona kabisa ni asilimia 9.3 na wenye matatizo ni 20.2.

Alisema tafiti zinaonyesha Zanzibar imezidi mara mbili zaidi ongezeko la wagonjwa wa macho kuliko Mkoa wa Kilimanjaro jambo ambalo linachangiwa na ukosefu wa elimu na kufuata masharti katika jamii‘

Daktari huyo aliwataka wataalamu hao kuzidisha utoaji wa elimu kwa wagonjwa hasa upimaji wa macho kwa wagonjwa wa sukari jambo ambalo litasaidia kupunguza ongezeko la Maradhi hayo.

Mgonjwa wa sukari anatakiwa kupata kipimo cha macho  kwa kila mwaka lakini kinyume na hapo mgonjwa wa sukari anaishi na sukari kwa muda wa miaka 20  hajawahi kupatiwa kipimo hicho jambo ambalo ni kosa ”alisema Dk.Kazim.

Dk.Kazim aliwataka madaktari hao wanapowapokea wagonjwa wa kisukari kuwapa elimu ya kutosha jinsi ya kutekeleza masharti ikiwemo utaratibu wa utumiaji wa dawa mfumo wa ulaji pamoja na kufanya mazowezi ili kuzuwia ongezeko la  sukari ambalo hupelekea kupoteza nuru ya macho .

Nae Kaimu Meneja wa Kitengo cha Maradhi yasio ambukiza Omar  Abdalla Ali kutoka Hospitali ya Mnazi mmoja amesema athari zinazotokana na maradhi ya sukari ni kubwa hivyo iko haja ya kuwajengea uwezo madaktari wa Vituo vya Afya ili kugundua mapema waliopata maradhi yasioambukiza na kufuata masharti ya dawa .

Mafunzo ya maradhi ya kisukari yanavyosababisha kutoona ni ya siku tatu yenye lengo la kupanga mikakati ya kupunguza ongezeko la maradhi yasioambukiza na jinsi ya kupambana nayo katika jamii yaliyongozwa na Dakatari Bingwa kutoka Tanzania.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.