Habari za Punde

Wabunge Kutoka Nchini Kenya Wakiwa Zanzibar Kwa Ziara na Michezo na Wenyeji Wao Baraza la Wawakilishi Zanzibar.





Baadhi Wabunge kutoka nchini Kenya  wakiwa Zanzibar katika ziara ya mapumziko ya kimichezo wakiwa wageni wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakitembelea shamba la viongo Kizimbani na kupiga picha za kumbukumbu ya ziara yao katika shamba la viungo wakimpiga picha mkwezi wa mnazi maarufu katika wa jina la Bauterfly, wakitembelea vivutio vya utalii katika mashamba ya viungo Kijichi Zanzibar.

Wabunge kutoka nchini Kenya  Waliopo Zanzibar kwa ajili ya michezo na mapumziko wakipatiwa madafu kwa ajili ya kuonja matunda yaliyopo zanzibar katika mashamba ya viungo Kijichi.

Wabunge kutoka nchini Kenya  waliopo Waliopo Zanzibar kwa ajili ya michezo na mapumziko wakifuatilia kwa umakini mkubwa maelezo ya waongoza wageni ambao hawapo katika picha wakifurahia na kupiga picha katika  vivutio vya utalii katika mashamba ya viungo Kijichi.
Wabunge kutoka nchini Kenya  waliopo Waliopo Zanzibar kwa ajili ya michezo na mapumziko wakifuatilia kwa umakini mkubwa maelezo ya waongoza wageni  katika  vivutio vya utalii katika mashamba ya viungo Kijichi.
Baadhi ya wachezaji wa mpira wa miguu timu ya wabunge kutoka kenya wakifatilia mchezo wao waliocheza na timu ya KMKM veterani uliofanyika katika uwanja wa Mao Zedong ambapo timu ya wabunge imeweza kuwaonesha ubabe mabaharia hao kwa kuwafunga goli moja kwa sifuri.
Mwenyekiti wa baraza la wawakilishi Zanzibar mhe Mwanaasha khamis Juma akiikagua timu ya mpira wa  vollyball  ya wabunge wa nchi ya Kenya wakati walipocheza mchezo wao kati ya timu ya mafunzo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.