Na.Mwashungi Tahir Maelezo 2-7-2021.
WAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais Kazi,Uchumi na Uwekezaji Mudrik Ramadhani Soraga ametoa taarifa rasmi kila ifikapo tarehe 3 siku yaJumamosi ya Mwanzo ya Mwezi wa Julai ya kila mwaka, ni Siku ya Ushirika Duniani.
Akitoa tamko ndani ya vyombo vya habari amesema Maadhimisho yatafanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul Wakil Kikwajuni Zanzibar siku iliyoteuliwa na Shirikisho la vyama vya Ushirika Duniani (International Cooperative Allience) mwaka 1923, na ilitangazwa rasmi na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa tarehe16 Disemba Mwaka 1992,ambapo wanaushirika huadhimisha.
Amesema madhumuni makuu ya kuadhimisha ni kutoa fursa ya kuhamasishana na kupeana elimu miongoni mwa wanachama juu ya dhana na umuhimu wa vyama vya ushirika kwa maendeleo yao kiuchumi na kijamii.
Pia kuimarisha ubia na mashirikiano miongoni mwa Mashirikisho ya Vyama vya Ushirika kati ya nchi mbalimbali , kwenye shirikisho la Ushirika la Kimataifa (International Cooperative Allience (ICA).
Vile vile kuwapa fursa wanaushirika katika nchi zao kutathmini mafanikio na kuendeleza changamoto pamoja na kuandaa mikakati ya kuendeleza vyamahivyo katika nchi zao.
Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kuyatekeleza maelekezo mbali mbali yanayotolewa na Jamhuri ya Kimataifa ikiwemo pendekezo la Shirika la Kazi Duniani (ILO Recommendation 193) juu ya kuendeleza na kusimamia vyama hivyo.
Aidha Zanzibar inaungana na wanaushirika walioko Mataifa mengine duniani kuadhimisha kwa misingi ya kutathmini mchango wa vyama vya ushirika, katika kutatua matatizo ya msingi ya kiuchumi na kijamii ya wanachama kwa misingi Uhiari na kidemokrasia.
Amesema kuwapa fursa wanaushirika kupima jinsi vyama vyao vinavyoendeshwa kwa kuzingatia misingi na kanuni za Kimataifa, Uzingatiaji wa Haki za Binaadamu, Usawa miongoni mwa wanachama na Utawala Bora,kutafakari kwa kiasi gani vyama vinafuata miongozo ya Sera ya Maendeleo ya Ushirika ya mwaka 2014,Sheria ya vyama vya Ushirika ya (2018) na kanuni zake.
Hata hivyo amesema kushajihisha Mshikamano na Demokrasia katika vyama , kuweka mikakati ili vichangie kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo Zanzibar ya mwaka 2020-2050 . malengo ya Maendeleo endelevu (SDGs) katika kuondosha njaa, kuimarisha viwanda vya kiushirika, ubunifu,kushiriki katika uchumi wa bluu na kutekeleza ajenda ya Afrika 2063.
Ujumbe wa mwaka huu 2021 ni “ Kwa pamoja Tujenge Ushirika” Maudhui ya ujumbe huo ni kushajihisha sekta zote katika jamii, kutekeleza juhudi za makusudi ili kuhakikisha kuwa vyama vinatatua mahitaji ya wanachama wao pia vinatoa ajira kwa makundi yote yakiwemo vijana, wanawake na watu wenye ulemavu na wazee.
“Natoa wito kwa wananchi tujiunge au tuanzishe vyama vya ushirika katika maeneo tunayoishi ili kwa pamoja tushiriki hatika harakati za kuichumi kwa maslahi yetu na kuijenga nchi yetu”,alisema Waziri Mudrik.
No comments:
Post a Comment