Habari za Punde

Hafla ya makabidhiano ya Ofisi ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais yafanyika leo

Waziri wa Nchi (OMKR) Saada Mkuya Salum akizungumza na watendaji wa Ofisis hiyo kuhusu umuhimu wa mashirikiano katika kazi mara baada ya  makabidhiano ya Ofisi ya Katibu Mkuu katika Ofisi  hiyo, hafla  iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Kilimani Mjini Unguja.
Waziri wa Nchi (OMKR) Saada Mkuya Salum akizungumza na watendaji wa Ofisis hiyo kuhusu umuhimu wa mashirikiano katika kazi mara baada ya  makabidhiano ya Ofisi ya Katibu Mkuu katika Ofisi  hiyo, hafla  iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Kilimani Mjini Unguja.
Aliyekuwa Katibu Mkuu (OMKR) Khadija Khamis Rajab akitoa neno la shukurani kwa watendaji wa Ofisi hiyo  katika hafla ya makabidhiano ya Ofisi ya Katibu Mkuu iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Kilimani Mjini Unguja.
Aliyekuwa Katibu Mkuu (OMKR) Khadija Kamis Rajab (kushoto) akimkabidhi nyaraka na vitabu mbalimbali Katibu Mkuu (OMKR) Omar Dadi Shajak (kulia) ikiwa na maana ya kumkabidhi Ofisi hiyo rasmi, hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Kilimani Mjini Unguja. Katikati ni Waziri wa Nchi (OMKR) Saada Mkuya Salum.
Katibu Mkuu (OMKR) Omar Dadi Shajak akizungumza na watendaji wa Ofisi hiyo mara baada ya makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano katika Ofisi ya (OMKR) iliyopo Kilimani Mjini Unguja.

Waziri wa Nchi (OMKR) Saada Mkuya Salum akimkaribisha rasmi Katibu Mkuu (OMKR) Omar Dadi Shajak katika Ofisi za Makamo wa Kwanza wa Rais zilizopo Kilimani Mjini Zanzibar.

PICHA NA FAUZIA MUSSA /MAELEZO ZANZIBAR


Na   Mwashungi Tahir Maelezo     

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa  Rais Dr Saada Mkuya Salum amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kutekeleza vyema majukumu yao ili kufikia lengo lililokusudiwa na  Serikali la kutoa huduma bora kwa wananchi.

Ameyasema hayo huko katika ukumbi wa Ofisi hiyo iliyoko Migombani wakati wa makabidhiano ya Ofisi kwa makatibu wakuu na kuwataka kushirikiana katika utendaji wa kazi na kuwakaribisha na kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Amesema muelekeo wa kazi katika wizara hiyo unakwenda vizuri hivyo amewasisitiza kuwa nae karibu katibu mpya katika kutekeleza majukumu ya Serikali ambapo inahimiza kila mfanyakazi kufanya kazi zake kwa ufanisi.

Aidha amemshukuru katibu anaeondoka kwa alivyofanya kazi zake kwa na kumuomba anakokwenda akayatimize wajibu na uimara wake kama alivyoyafanya hapo.

Nae Katibu Mkuu Kazi na Uwezeshaji Khadija Khamis Rajab amesema kwa muda aliofanya kazi katika Wizara hiyo ameweza kurekebisha mambo mengi kwa mashirikiano aliyoyapata baina yake na wafanyakazi hao.

Hivyo amesema ameweza kupata mafanikio kwa kupata ofisi ambapo hapo mwanzo kulikuwa kuna ufinyu na kuweza kupunguza baadhi ya madeni ya wafanyakazi yakiwemo wanayodai  pesa za likizo na mambo mengineo.

Aidha amewahimiza wafanyakazi kumpa mashirikiano makubwa ili aweze kupata urahisi wa utendaji wa kazi katika majukumu yake.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamo wa kwanza wa Rais Omar Dadi Shajack ameahidi kufanya kazi kwa mashirikiano ili majukumu ya kazi yaweze kuendelea ikiwemo uwajibikaji kwa kila mmoja.

“Tushirikiane katika uwajibikaji kwa kila mmoja anapotoka nyumbani akija kazini ajuwe anakuja kufanya kazi zake hadi anapoondoka,”alisisitiza katibu huyo.

Pia amewataka kujiwekea ubunifu na kupanga mikakati ya kazi kwa lengo kukuza uwajibikaji katika nafasi zao za kazi ili  ziweze kuimarika zaidi.

Vile vile Katibu Sharjach amesema maagizo ya Awamu ya Nane ya Rais Dkt Mwinyi ni kukuza  spidi ya kazi ili malengo anayoyahimiza yaweze kufikiwa kwa kuimarisha utendaji.   



 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.