Habari za Punde

Raza adhamini vifaa vya michezo kwa ajili ya Tamasha la Utamaduni wa Mzanzibari litakalofanyika Pemba

Waziri wa Habari ,Vijana, Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita akipokea Vifaa vya Michezo vitakavyotumika katika mchezo utakaowakutanisha Maveterani wa Mpira wa miguu utakaochezwa katika Uwanja wa Gombani Chakechake Pemba katika maadhimisho ya Tamasha la Utamaduni wa Mzanzibar agosti 29 mwaka huu.

Mveterana Ahmed Mwanga mstaafu wa mchezo wa  GOSIP aliechukua ushindi Nchini Uganda mara mbili mnamo mwaka 1963 katika mchezo huo akizungumza kuhusu nidhamu katika michezo wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo vilivyotolewa na Mfanya Biashara maarufu Zanzibar Mohammed Raza.

PICHA NA BAHATI HABIBU / MAELEZO ZANZIBAR.


Na Ali Issa Maelezo 4/8/2021 .

Waziri wa Habari Vinaja Utamaduni na Michezo, Tabia Maulid Mwita amesema Wizara ya Habari imeamua kurudisha hadhi ya michezo  Zanzibar, ili kuona sekta hiyo inafanikiwa  kitaifa na kimataifa.

Hayo ameyasema leo huko Wizarani kwake Migombani wakati akipokea msaada wa vifaa vya michezo ikiwemo Jezi, vikombe nishani za Dhahabu na Fedha kutoka kwa Mfanyabiashara maarufu Muhamed Raza ili kufanikisha mashindano ya wana michezo wastaafu (VETERAN) yanayotarajiwa kufanyika Pemba Uwanja wa Gombani katika kilele cha Tamasha la utamaduni tarehe 29 mwezi huu.

Amesema amepokea msaada huo kwa mikono miwili, kwa furaha kubwa na kusema kuwa msaada huo ni dhahiri kuwa mfadhili huyo ni mzalendo anaeipenda nchi yake.

Amesema kwa muktadha huo,  mashindano ya vetirani  yatafanyika bila wasiwasi na shauku kubwa Kwani wameshakamilisha ufanikishaji wa mchezo huo.

Amesema wazee ndio chimbuko la kuiletea Zanzibar nishani mbali mbali hivyo na wao lazima waoneshe uwezo wao walivyo weza kuitumikia Zanzibar  katika sekta ya michezo.

Alisema mpambano huo utawakutanisha wazee wa Unguja na Pemba bilashaka mchezo huo utakuwa na mwamko mkubwa.

Aidha alisema michezo ni sehemu ya utamaduni, hivyo ni vyema tamasha hilo likamilike kwa mchezo huo wa wazee walio ng’ara miaka iliopita, na utaonyeshwa moja kwa moja na ZBC tv.  

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo Muhamed Raza amesema ametoa msaada huo baada ya kupelekewa ombi na Wizara hiyo, hivyo hakunabudi kutoa vifaa hivyo ili kufanikisha michezo huo.

Aidha alisema kuwa yeye ni Mzalendo anae penda Zanzibar yuko tayari kuisaidia Serikali ya Zanzibar wakati wowote kwa suala la michezo na mambo mengine mbalimbali.

Amesema amefurahishwa mno kuona kuwa Wizara imeona umuhimu wa Veterani kupewa nafasi ya kuonesha vipaji vyao katika tamasha hilo.

 Nao Wazee magwiji wa mpira Abdalla Maulid na Ahmada Mwanga walisema kuwa sikuu hiyo wataonyesha kabumbu kabambe la kuwafurahisha wapenda mechezo kama vile ilivyo kuwa wakati walipo kuwa wakikipiga KMKM na Malindi miaka 42 iliopita.

Walisema wao watakuwa tayari kutoa michango yao iwapo watahitajika kuisaidia serikali ili kuona kuwa michezo inakuwa Zanzibar.    

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.