Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wakati alipowasili kwenye viwanja vya Chuo cha Kyela Polytechnic College kutembelea Chuo hicho, Agosti 2, 2021. Kutoka kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanachuo wanaoseomea taaluma ya ususi wakati alipotembelea Chuo cha Kyela Polytechnic College Agosti 2, 2021. Wa tatu kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na wanachuo wa Chuo cha Kyela Polytechnic College College wakati alipotembelea Chuo hicho, Agosti 2, 2021. Kulia kwa Waziri Mkuu ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako na kushoto kwa Waziri Mkuu ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama shati la kitenge lililoshonwa na Wanachuo wa Chuo cha Kyela Polytechnic College wakati alipotembelea Chuo hicho
Moja kati ya majengo ya Chuo cha Kyela Polytechnic College ambacho Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikitembelea, Agosti 2, 2021.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment