Habari za Punde

Zaidi ya Milioni Mia Tisa Zakusanywa Katika Harambee ya Kusaidi Ligi Kuu ya Zanzibar.

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akihutubia wakati hafla ya uzinduzi wa Harambee ya kuchangia Udhamini na Ufadhili wa Ligi Kuu ya Mpira wa Miguu Zanzibar kwa msimu wa mwaka 2021/2022, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahr Mbweni Jijini Zanzibar usiku wa 15/8/2021. na (kulia )Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Tabia Maulid Mwinyi na Rais wa ZFF Ndg.  

Na.Kassim Abdi.OMPR.

Jumla ya shilling Million Mia Tisa na Arubaini, laki tano  Elfu kumi (940,510,000) zimekusanywa katika harambee maalum ya kuchangia Ligi kuu ya Zanzibar ikiwa ni jitihada za kuinua Sekta ya Michezo Nchini.

Harambee iyo imeendeshwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla iliofanyika katika hotel ya Madinatu Al bahri Mbweni  iliowashirikisha wadau mbali mbali wa michezo kutoka taasisi za serikali na taasisi za watu binafasi.

Akihamasisha zoezi hilo la harambee la kuchangia ligi kuu ya Zanzibar  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla alisema katika maeneo yaloiyopewa kipaumbele na serikali ya awamu ya nane ni kurejesha hamasa ya michezo nchini ili kuitangaza Zanzibar kitaifa na kimataifa kupitia sekta ya michezo.

Alisema Rais Dk. Mwinyi  ni mdau namba moja wa michezo ambapo kupitia hotuba zake mbali mbali ameahidi kupitia serikali nanayoiongoza itatoa kila aina ya ushirikiano katika kuhakikisha michezo hasa soka la mpira wa miguu inapata ushawishi mkubwa kwa lengo la kuinua mchezo huo, na kuibua vipaji  vya  Wazanziabri.

Alieleza kuwa,  wapo wachezaji kadhaa wa mpira wa miguu kutoka Zanzibar  wamekuwa kielezo chama cha maenedeleo ya soka  kwa kusajiliwa katika timu za Tanzania bara na pamoja na kuitwa katika timu ya Taifa na kutoa ishara kuwa ni miongoni mwa matunda  yanaonekana kwa kuibua vipaji tofauti.

Mhe. Hemd aliwapongeza na kuwashukur wadau wote waliojitokeza kuunga mkono juhudi hizo za serikali  na ameendlea kuwakaribisha wadau wengine wa ndani na nje ya nchi kujitokeza nao kufadhili ligi kuu ya Zanzibar.

Katika Harambee hiyo Makamu wa Pili wa Rais alipokea michango kutoka taasis mbali mbali kwa njia ya simu ikiwemo kampuni ya GSM ambayo ilichangia jumla ya Millioni Hamsni kwa niaba ya Klabu ya Yanga na kutoa wito kwa klabu nyengine Nchini kujitokeza kuchangia kwani milango bado itaendelea kuwa wazi.

Aidha Mhe. Hemed aliutaka uongozi wa wizara ya habari vijana utamaduni na michezo pamoja na shirikisho la mpira wa miguu Zanzibar (ZFF) kuhakikisha mchango huo unatumika kwa jambo lililokusudiwa sambamba na kuonya kuwa kuwa yoyote atakaefanya jambo kwa maslahi binafsi serikali hatovumiiwa.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi Waziri wa Habari vijana utamaduni na michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa maandalizi ya  harambee hiyo ni moja kati ya maelekezo ya Rais Dk Mwinyi  katika kuhakikisa ligi kuu ya Zanzibar  inapata ufadhili, ili kuirejesha hadhi ya michezo  ambazo Zanzibar ilikuwa ikitajika katika ukanda wa Afrika Mashariki.
 
Alismema  kuwa sera ya michezo imeelekeza kuinua sekta hiyo kwa kuandaa mashindamo ya kitaifa na kimataifa, hivyo amewatoa wasi wasi wapenzi wa soka nchini kuwa ligi kuu itakayoandaliwa  mwaka huu itafuata na kuzingatia sheria zote zilizoanishwa katika na sheria za soka .

Akitoa Salamu za Wizara ya habari vijana utamaduni na michezo Katibu  Mkuu Wizara hiyo Fatma Hamad Rajab alieleza wizara imejipanga vyema katika kuhakikisha azma ya serikali ya  Awamu ya Nane inayoongozwa na Rais Dk. Mwinyi inafikiwa, na kueleza kuwa wadhamini hao wameonesha utayari wao katika kuunga mkono juhudi hizo.

Nao Wadau  mbali mbali Wakichangia katika Harambee hiyo walieleza  kuwa serikali imeonesha dhamira ya kutaka kurejesha hadhi ya soka nchini nao wameona  vyema kwao kuongeza kasi ya ufadhili, ili kuona vipaji na uwezo wa vijana katika mpira wa miguu vinazalishwa zaidi.
 
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Agosti 15, 2021.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.