Habari za Punde

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa Atembelea Maonesho ya Sekta ya Mifungo Kwenye Mkutano wa Wadau Sekta Hiyo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla wakati alipowasili kwenye Kituo  cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Septemba 7, 2021 kufungua Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Mifugo
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama viatu wakati alipotembelea banda la kiwanda cha Kilimanjaro International Leather Industries Company Limited kilichopo eneo la   Karanga Moshi  kabla ya kufungua Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Mifugo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Septemba  7, 2021. Wa pili kulia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mkanda  uliotengenezwa na kiwanda cha Kilimanjaro International Leather Industries Company Limited kilichopo eneo la  Karanga Moshi wakati alipotembelea banda la kiwanda hicho  kabla ya kufungua Mkutano wa Wadau Sekta ya Mifugo kwenye Kituo  cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Septemba  7, 2021. Wa pili kulia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.