Habari za Punde

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia aagiza kufanywa tathmini ya kina ya vitu vilivyoungua jengo la Sayansi za Bahari, Forodhani


Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akitoa maelekezo ya namna ya ujenzi wa Maabara  ya Sayansi za Baharini huko katika maeneo ya Chuo hicho Buyu Wilaya ya  Magharibi Unguja.

Na Maulid Yussuf WEMA

Waziri wa Elimu Na Mafunzo ya Amali Zanzibar mhe Simai Mohammed Said  na Waziri wa Elimu sayansi na teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, wakiangalia kwa amakini madhara yaliyojitokeza ya kuungua moto kwa jengo laChuo Kikuu cha Dar Es salaam sayansi za Bahari kiliopo Forodhani Mjini Unguja, kufuatia juungua moto hivi karibuni.

Na Maulid Yussuf WEMA.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe, Simai Mohammed Said wa kwanza kushoto, akiwa na Waziri wa Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako wakipata maelezo juu ya madhara ya moto yaliyotokea katika jengo la Chuo Kikuu cha Dar es salaam Sayansi za Baharini liliopo Forodhani Mjini Unguja, wakati walipofika kuangalia madhara hayo.

Na Maulid Yussuf WEMA

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako wa Kwanza kulia akiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said wakipata maelezo juu ya madhara yaliyotokea ya kuungua moto jengo la Chuo Kikuu cha Dar ess salaam la sayansi za bahari liliopo Forodhani Mjini Unguja, wakati walipofika kuangalia madhara hayo.

Na Maulid Yussuf WEMA

Na Maulid Yussuf WEMA

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ameuagiza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es salam kupitia Taasisi ya Sayansi za Bahari kuharakisha wanafanya tathmini ya vitu  vilivyoungua moto  hivi karibu ili kupatiwa ufumbuzi.

Akizungumza baada ya kufanya ziara ya kuangalia athari ilizopata Taasisi za Sayansi ya bahari ya kuungua moto huko forodhani amesema kufanya hivyo ikutaiwezesha Serikali kutoa msaada wa haraka ili  Taasisi hiyo iweze kutoa elimu kwa Wanafunzi. 

 Profesa Ndalichako amewahakikishia Wanafunzi wa Chuo hicho kuwa Serikali itafanya kila jitihada ili kuhakikisha wanaendelea na masomo yao kama kawaida pamoja na kupata wataalamu wazuri hapa nchini. 

 

Ameefahamisha kuwa Wizara ya Elimu ya Tanzanzia bara na Zanzibar zinaendana na vipaumbele vilivyowekwa na Serikali zote mbili hasa kupitia uchumi wa buluu, hivyo kuwepo Taasisi hiyo ni muhimu sana kwa maendeleo ya malengo ya Serikali hizo.

Profesa Ndalichako, ametumia fursa hiyo kuwashukuru kikosi cha Zimamoto na uokozi cha Bandarini pamoja na wananchi wote walioshiriki kuuzima moto ili kuhakikisha maafa yaliyotokea hayaleti madhara zaidi.

Nae Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe, Simai Mohammed Said amesema amefarajika kutokana na ujio wa Mhe Ndalichako huku akimuahidi kuwa Wizara  itaendelea kushirikiana nae ili kuhakikisha masomo yanaendelea ndani ya Taasisi hiyo.

Nae Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Willium Mwanagishe amesema Chuo hicho kimejipanga kujenga maabara ya muda ili kuwarahisishia Wanafunzi Kusoma kwa wakati.

Zaidi ya shillingi  Billioni moja zinahitajika katika kukarabati jengo hilo lilopata ajali ya kuungua moto tarehe 2 mwezi huu.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.