Habari za Punde

Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Yatakiwa Kuwa ya Kimataifa -Mhe. Masoud.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman akikabidhiwa zawadi maalum inayoitangaza Benki ya Watu wa Zanzibar na Mkurugenzi Muendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Dk.Muhsin Suleiman Masoud na (kulia kwake) Meneja Masoko na Uendelezaji Bishara (PBZ) Ndg, Said Ali Mwinyigogo, hafla hiyo imefanyika katika Ofisi ya Makamu wa Kwanza Migombani Jijini Zanzibar.
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mh. Othman Masoud Othman akizungumza na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Dk. Muhusin Suleiman Masoud(kulia kwa makamu). Mkurugenzi huyo na ujumbe wake ulifika Ofisini kwa makamu leo kujitambulisha na kushauriana kuhusu masuala mbali mbali ya Benki. ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

MAKAMU Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman, amesema ni muhimu kwa Uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar ( PBZ) kuongeza ubunifu katika utoaji wa huduma  kuwa na kiwango cha kimataifa na zinazohimili ushindani wa biashara ya Fedha dunaini.

Mhe.Othman ameyasema hayo leo Ofisini kwake Mingombani mjini Zanzibar alipokutana na Uongozi wa Benki ya PBZ, uliofika ofisini kwa makamu kujitambulisha na kushauriana naye juu masuala mbali mbali kuhusu Benki hiyo.

Amesema hivi sasa Zanzibar kuna Benki nyingi zinazofanya kazi ya utoaji wa huduma za kifedha kwa wananchi na wageni jambo ambalo linaongeza ushindaji kwa kuwa wateja wengi wanaojiunga na huduma za benki zinazoanzishwa pia ndio  wanaohitajika na PBZ.

Aidha Makamu amesema kwamba pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na  uongozi wa Benki hiyo kuimarisha hudma, lakini bado zipo changamoto mbali mbali zikiwemo za urejeshaji wa mikopo kutoka kwa wateja wake pamoja na kuwepo mifumo ya kisheria ndani ya benki hiyo  inayohitaji kufanyiwa marekebisho  ili kwanda na wakati  wa ushindani wa biashara hiyo.

Alishauri  Uongozi wa PBZ kufanya marekebisho katika baadhi ya sheria ili kuimarisha taratibu zinazosimamia benki hiyo kwa nia ya kuweka mfumou bora zaidi wa utoaji wa huduma na kusaidia kuwavuta zaidi  wateja wake kuendelea kuitumia Benki hiyo .

Aidha aliutaka Uongozi wa Benk hiyo kuendelea kuitumia fursa ya Uzalendo wa Wananchi na Wafannyabiashara wa Zanzibar kuendelea kuipenda Benki yao kwa kupata huduma bora za Kibenki zitakazowaridhisha ili waendelee kuiamini kwamba ni benki bora kuliko zote zilizopo Zanzibar.

Naye Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Dk. Muhsin Suleiman Masoud, amesema kwamba pamoja na changamoto mbali mbali zilizopo katika Benki hiyo, lakini wamekuwa wakijitahidi kuimarisha utoaji wa huduma  bora ili kwenda na wakati na kuhimili ushindani.

Alikiri kwamba urejeshaji wa mikopo kutoka kwa baadhi ya wateja wake bado inaendelea kuwa changamoto kubwa  ambapo hali hiyo inapotokea mara nyengine huchangia gharama za mikopo kuwa kubwa kwa wateja wa aina hiyo.

Hata hivyo, Mkurugenzi huyo amesema kwamba licha ya Benki hiyo kupitia katika kipindi kigumu, lakini bado ipo vizuri na inaendelea kuimarika na wateja wengi wanapenda kutumia huduma za Benki hiyo.

Amefahamisha kwamba hivi karibuni Benki hiyo itaendelea kufungua matawi mapya katika mikoa kadhaa ya Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na kuongeza mawakala hadi 800 kutoka 200 walipo sasa. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.