Habari za Punde

Makamu wa Rais Mhe Mpango Akabidhi Zawadi ya Krismass Kwa Watoto wa Kituo cha Poloni Kondoa Dodoma.

 

Msaidizi wa Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Emma Liwenga  Akimkabidhi zawadi mbalimbali  kwaajili ya Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya kwa kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Sister Restituta Jovin ambaye ni Mkuu wa Kituo cha Kulea Watoto yatima cha Poloni kilichopo Kondoa mkoani Dodoma. 

Watoto wa kituo cha kulea watoto yatima cha Poloni kilichopo Kondoa mkoani Dodoma wakisali pamoja na Msaidizi wa Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Emma Liwenga  mara baada ya kukabidhiwa zawadi mbalimbali za sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya zilizotolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Desemba 24,2021.

Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo tarehe 24 desemba 2021 amekabidhi zawadi mbalimbali za sikukuu za Krismasi na mwaka mpya katika kituo cha kulea watoto yatima cha Poloni kilichopo Kondoa mkoani Dodoma.

Akikabidhi kwa niaba ya Makamu wa Rais, msaidizi wa Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Emma Liwenga amesema zawadi hizo ni katika kukidhi mahitaji ya watoto hao kipindi hiki cha sikukuu. Amesema Makamu wa Rais ametuma salamu za Upendo na kuwaomba watoto hao kukua katika maadili.

Aidha Dkt Emma amesema Makamu wa Rais amewashukuru waangalizi wa watoto hao kwa kujitoa kwao kuwalea katika maadili mema na kuomuomba Mungu kuendelea kuwabariki Masista na wahudumu wengine katika malezi yao kwa watoto hao.

Kituo hicho cha Poloni kilianzishwa Mwaka 1947 na mpaka sasa kina jumla ya watoto 46 ambao wanapokelewa kuanzia umri wa siku moja tangu kuzaliwa.

Zawadi zilizokabidhiwa ni pamoja na Mchele, Unga wa Ngano, Sabuni, Sukari, Mafuta, vinywaji pamoja na mbuzi wawili.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.