Habari za Punde

Serikali Yaongeza Bilioni 6 Kukamilisha Ujenzi wa Nyumba za Wanangorongoro.

 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na wananchi wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa(Mb) (hayupo pichani) katika eneo la makazi mapya ya Wanangorongoro kwenye Kijiji cha Msomera Wilayani Handeni Mkoani Tanga.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula (Mb) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb)(kulia) wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (hayupo pichani) alipofanya ziara katika eneo la makazi mapya ya Wanangorongoro kwenye Kijiji cha Msomera Wilayani Handeni Mkoani Tanga.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (wa pili kushoto) akijadili jambo na viongozi wengine wa Serikali wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (hayupo pichani)katika eneo la makazi mapya ya Wanangorongoro kwenye Kijiji cha Msomera Wilayani Handeni Mkoani Tanga.

Serikali imetenga fedha kiasi cha shilingi bilioni 6 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa nyumba 400 kwa ajili ya wananchi wanaoishi katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ambao wako tayari kuhamia kwenye makazi mapya yanayojengwa Kijiji cha Msomera Wilayani Handeni Mkoani Tanga.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotembelea Kijiji cha Msomera Wilayani Handeni.

“Mhe. Waziri Mkuu nikuhakikishie kwamba kwa kuwa tumeanza huu mradi wa kujenga nyumba ambapo 103 tayari zimekamilika, tumepata fedha tena kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kiasi cha shilingi bilioni 6 hivyo tutajenga nyumba nyingine 400 kwa ajili ya kuhakikisha wenzetu waliokubali kuhama kwa hiari kuja kuishi na binadamu wenzao ” Mhe. Masanja amesisitiza.

Amesema ni hatari sana kwa binadamu kuendelea kuishi na wanyama wakali na waharibifu na kuwashauri wanangorongoro kukubali wito wa kuhamia kijiji cha Msomera.

“Maisha ya kuchanganyikana na wanyama yana hatari kubwa hasa kwa watoto ambapo wanashindwa kwenda shule kwa sababu wanahofia kukutana na wanyama wakali kama Simba.

Amefafanua kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameamua kuwasaidia wana ngorongoro kwa kuwa eneo hilo litakuwa na huduma zote za msingi na litakuwa ni eneo la mfano.

Aidha, amesema kuwa wanangorongoro watajiendeleza kiuchumi wakiwa katika eneo makazi hayo mapya kwa sababu walipo sasa Ngorongoro wanabanwa na sheria ambazo haziwaruhusu kumiliki ardhi, kulima na kufanya shughuli yoyote ile zaidi ya kuchunga sasa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.